• HABARI MPYA

  Saturday, May 31, 2014

  KUNDI LA MBEYA CITY NOMAAA MICHUANO YA MIPYA YA CECAFA...AFC LEOPARD, ACADEMIE TCHITE ZATINGA NUSU FAINALI

  Wachezaji wa Academie Tchite ua Burundi wakishangilia baada ya kuitoa El Merreikh ya Sudan katika Robo Fainali ya michuano ya Nile Basin usiku wa jana mjini Khartoum kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90. 
  Mashabiki wa Merreikh wakiwa wenye majonzi baada ya timu yao kutolewa katika michuano hiyo ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), inayoshirikisha mabingwa wa Kombe la FA au washindi wa pili wa Ligi Kuu za nchi wanachama wa baraza hilo
  Wachezaji wa AFC Leopards ya Kenya wakishangilia baada ya kuitoa Defence ya Ethiopia kwa mabao 3-2. Leopards na Tchite zote zilikuwa kundi B pamoja na Mbeya City, ambayo inacheza na Victory University ya Uganda katika Robo Fainali nyingine, huku Al Shandy ikimenyana na Malakia ya Sudan Kusini.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KUNDI LA MBEYA CITY NOMAAA MICHUANO YA MIPYA YA CECAFA...AFC LEOPARD, ACADEMIE TCHITE ZATINGA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top