• HABARI MPYA

  Saturday, May 24, 2014

  NGORONGORO HEROES YAIVAA NIGERIA LEO

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  Kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) leo kinashuka uwanjani nchini Nigeria kuivaa Nigeria (Flying Eagles) katika mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika.
  Kikosi cha Ngorongoro kilichofungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam 

  Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Ahmadou Bello uliopo katika Jimbo la Kaduna kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa za Nigeria. Ngorongoro Heroes ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0.
  Mwamuzi Alhadi Allaou Mahamat wa Tchad ndiye atakayechezesha mechi hiyo. 
  Atasaidiwa na Issa Yaya, Alfred Madjihoudel na Idriss Biani wote kutoka Tchad. Kamishna ni Aboubakar Alim Konate wa Cameroon. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YAIVAA NIGERIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top