• HABARI MPYA

  Thursday, May 29, 2014

  BREAKING NEWS: NTEBE WA MTIBWA AMWAGA WINO RUVU SHOOTING

  Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM 
  ALIYEKUWA mchezaji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Salvatory Ntebe amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Ruvu Shooting ya Pwani.
  Masau Bwire, Msemaji wa Ruvu Shooting, ameiambia BIN ZUBEIRY muda mfupi uliopita kuwa Ntebe, ambaye hucheza kama beki wa kati, amesaini mkataba huo leo saa 8 alasiri kenye ofisi za klabu hiyo Mlandizi, Pwani.
  Ntebe anakuwa mchezaji wa pili kutoka kwa mabingwa wa Tanzania Bara 1999 na 2000 -- Mtibwa Sugar kusajiliwa na Ruvu Shooting msimu huu akitangiliwa na Juma Mpakala aliyesaini miaka miwili ikiwa ni sehemu ya mikakati ya timu hiyo kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao.
  Anahamia jeshini; Salvatry Ntebe ni beki ambaye alikuwa akizivutia hata timu kubwa

  Mbali na kuichezea Mtibwa, Ntebe aliwahi pia kuzitumikia timu za Atletico ya Ligi Kuu Burundi, AFC ya Arusha, Azam FC na Kagera Sugar.
  Wachezaji wengine waliosajiliwa na Ruvu Shooting kwa maagizo ya kocha mkuu wa timu hiyo ni Zuberi Dabi kutoka Kagera Sugar na mshambuliaji Mtanzania Chagu Chagula aliyekuwa akikipiga katika klabu ya Muzinga ya Ligi Kuu Burundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BREAKING NEWS: NTEBE WA MTIBWA AMWAGA WINO RUVU SHOOTING Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top