• HABARI MPYA

  Saturday, May 24, 2014

  YAYA TOURE APATA UGONGWA USIOELEZEKA, AENDA KUTIBIWA UARABUNI IVORY COAST IKIWEKA KAMBI MAREKANI

  KIUNGO Yaya Toure anapatiwa matibabu nchini Qatar kwa maumivu ambayo hayajawekwa wazi kabla ya kuungana na wachezaji wenzake wa Ivory Coast katika iambi yao ya kujiandaa na Kombe la Dunia nchini Marekani, imesema taarifa ya Shirikisho la Soka Ivory Coast jana.
  Ni mchezaji pekee katika kikosi cha awali cha wachezaji 28 kilichoteuliwa na kocha Sabri Lamouchi aliyekosa hatua za mwanzo za maandalizi ya Kombe la Dunia mjini Dallas kuanzia juzi.
  Kiungo huyo atasafiri kwenda Marekani Alhamisi ijayo kuungana na wenzake, imesema taarifa ya shirikisho.
  Hofu: Yaya Toure anapatiwa matibabu ya maumivu ambayo hayajawekwa wazi kabla ya kwenda kuungana na wenzake kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia

  Hospitali ya tiba za wanamichezo, Aspetar Orthopaedic mjini Doha imethibitisha kumpatia tuba Mwanasoka huyo bora wa Afrika katika taarifa iliyosema anasumbuliwa na 'majeruhi madogo'.
  Toure aliumia mguu katikati ya Aprili, lakini akapona baada ya wiki mvili na kurejea uwanjani kuisaidia Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
  Katika siku ya mwisho ya msimu wa ligi hiyo, Mei 11 alitolewa nje kipindi cha pili na taaruifa zikasema alipata maumivu ya nyama City ikiifunga West Ham.
  Maandalizi ya Toure kuelekea Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika kati ya Juni na Julai nchini Brazil, yamefunikwa na maelezo ya wakala wake, Dimitri Seluk wiki hii aliyesema kwamba kiungo huyo amesikitishwa na City kutojali kuhusu birthday yake na anaweza kuwahama mabingwa hao wa England.
  Ivory Coast watacheza mechi mvili za kujipima nguvu nchini Marekani, dhidi ya Bosnia mjini St Louis Mei 30 na El Salvador mjini Dallas Juni 4 kabla ya kuwasili Brazil Juni 6, ambako wamepangwa Kundi C pamoja na Colombia, Ugiriki na Japan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YAYA TOURE APATA UGONGWA USIOELEZEKA, AENDA KUTIBIWA UARABUNI IVORY COAST IKIWEKA KAMBI MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top