• HABARI MPYA

    Tuesday, May 27, 2014

    LUKAKU APIGA HAT TRICK UBELGIJI IKIUA 5-1 JANUZAJ NDANI

    KIUNGO wa Manchester United, Adnan Januzaj ameichezea mechi ya kwanza Ubelgiji Jumatatu usiku ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Luxembourg katika mchezo wa kirafiki ambao mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku alifunga mabao matatu.
    Januzaj, mwenye umri wa miaka 19, alichagua kuchezea Ubelgiji mwezi uliopita licha ya kwamba ana asili ya Albania, Kosovo, na haya England.
    Saluti: Lukaku amepiga hat-trick yake ya kwanza akiwa na jezi ya Ubelgiji katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Luxembourg

    Lukaku alifunga bao la kwanza dakika ya tatu, akimalizia pasi ya Marouane Fellaini. Joachim aliisawazishia Luxembourg dakika ya 13, lakini Lukaku akaifungia Ubelgiji bao la pili dakika 10 baadaye.
    Nyota wa United, Januzaj alichezea mechi yake ya kwanza kikosi cha Ubelgiji akitokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Marc Wilmots, huku Vincent Kompany na Eden Hazard wakipumzishwa.
    Red Devil: United man Adnan Januzaj opted to play for Belgium last month
    Kishetani Chekundu: Mchezaji wa Man United, Adnan Januzaj aliamua kuchezea Ubelgiji mwezi uliopita

    And Lukaku, ambaye alikuwa kwa mkopo Everton msimu uliopita, alikamilisha mabao yake matatu kabla ya Nacer Chadli kufunga la nne na Kevin De Bruyne kufunga la tano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LUKAKU APIGA HAT TRICK UBELGIJI IKIUA 5-1 JANUZAJ NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top