• HABARI MPYA

  Monday, May 26, 2014

  AZAM AKADEMI WAWAHISHWA KAMBINI MASHINDANO JULAI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI wa timu ya akademi ya Azam FC wataripotia kambini Juni 25, mwaka huu kuanza maandalizi ya mashindano ambayo yatafanyika Julai mwaka huu.
  Taarifa ya Azam FC katika tovuti yake imesema kwamba, kutokana na mabadiliko ya tarehe za mashindano yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Julai, mwaka huu sasa wachezaji wa akademi wataripoti kambini Juni 25, badala ya Agosti 6 kama ilivyopangwa awali.
  Kevin Friday kushoto ni moja ya matunda ya akademi ya Azam FC

  Aidha, taarifa hiyo pia imesema kwamba usaili wa vijana wanaotaka kujiunga na akademi ya mabingwa hao wa Bara utafanyika Julai 1, mwaka huu kuanzia Saa 1: 30 asubuhi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Taarifa imesema usaili huo utahusisha vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 17 na wote wapendao kujaribu bahati yao wametakiwa kufika kabla ya Saa 1.00 asubuhi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM AKADEMI WAWAHISHWA KAMBINI MASHINDANO JULAI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top