• HABARI MPYA

  Friday, May 23, 2014

  ADEBAYOR AWAPONDA IVORY COAST KUCHEZA 'KIFAZA' HAWATAFANYA LOLOTE KOMBE LA DUNIA, AWEKA DAU KWA NIGERIA

  MSHAMBULIAJI wa Tottenham, Emmanuel Adebayor amewashambulia Yaya Toure na wachezaji wenzake wa Ivory Coast kwa kujaribu lusaka ushujaa binafasi badala ya kucheza pamoja kama timu.
  Mshambuliaji huyo wa The Togo anakerwa sana na kikosi cha Tempo wa Ivory Coast kuwa na nyota wa Ligi Kuu ya England kama Kolo Toure, Cheick Tiote na Wilfried Bony, sambamba na wakali wengine kama Didier Drogba na Gervinho, lakini haifanyi vizuri.
  "Sijawahi kuwaamini wao. Ni nchi ambayo wakati inakuangusha," alisema Adebayor akizungumza na mtandao wa Ghana, SoccerNet.

  Wanatuangusha: Emmanuel Adebayor (chini) amewashutumu nyota wa Ivory Coast kwa kutocheza kitimu
  Blast: The Spurs striker said the team need to play together and not all try and be heroes
  Shutuma: Mshambuliaji wa Spurs amesema Ivory Coast inahitaji kucheza kitimu

  Amesema; "Inakuwaje kwa miaka mine au mitano iliyopita hawajashinea Kombe la Mataifa ya Afrika? Wana washambuliaji wazuri Ulaya kama Didier Drogba. Wana viungo bora leo, Yaya Toure. Una mmoja wa washambuliaji bora kwenye ligi leo, Wilfried Bony. una wachezaji wote hao.
  "Lakini suala ni kwamba, watakwenda kuwajibika kwa pamoja kiasi cha kutosha? Sijui. Mimi siyo mu Ivory Coast. Watakuwa wanazungumza, kucheza na kufurahia pamoja, lakini wakati unapofika wanasahu kazi yao,".
  Adebayor anaipa nafasi Nigeria kufanya vizuri kati ya wawakilishi wote watano wa Afrika, kwa sababu wamedhamiria, wakayti Ghana, ambao kikosi chao kinaundwa na wachezaji wa Ulaya watupu , kama Ivory Coast, wanamtegemea Asamoah Gyan.
  Best chance: Adebayor believes Nigeria have the best chance in Brazil because they are the most organised
  Nafasi nzuri: Adebayor anaamini Nigeria bwana nafasi ya kufanya vizuri Brazil kuliko timu nyingine yoyote ya Afrika
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ADEBAYOR AWAPONDA IVORY COAST KUCHEZA 'KIFAZA' HAWATAFANYA LOLOTE KOMBE LA DUNIA, AWEKA DAU KWA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top