• HABARI MPYA

  Sunday, May 25, 2014

  BALOTELLI KUREJEA ENGLAND NA HUENDA AKATUA LIVERPOOL AU ARSENAL, ITATEGEMEA

  MSHAMBULIAJI Mario Balotelli anajiandaa kurejea Ligi Kuu ya England msimu ujao katakana na Arsenal na Liverpool kupigania saini yake.
  Nyota huyo wa AC Milan amechoshwa na tania za kibaguzi Italia na inafahamika mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City amekiri maisha ya England hayakuwa mabaya.
  Arsenal wapo kwenye mazungumzo na Real Madrid kwa ajili ya kumsaini Karim Benzema lakini watazungumza na watu wa Balotelli pia.
  Liverpool itamfuata Balotelli iwapo Luis Suarez atakubali of a ua kujiunga na Real Madrid au Barcelona baada ya Kombe la Dunia.
  Atarudi? Mario Balotelli anaweza kurejea Ligi Kuu Engand kupitia Liverpool au Arsenal
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALOTELLI KUREJEA ENGLAND NA HUENDA AKATUA LIVERPOOL AU ARSENAL, ITATEGEMEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top