• HABARI MPYA

  Friday, May 30, 2014

  TEDDY SHERINGHAM AREJEA WEST HAM

  KLABU ya West Ham imethibitisha kumteua Teddy Sheringham kuwa kocha wa washambuliaji wa timu hiyo ya Upton Park.
  Kocha Sam Allardyce ameambiwa ahakikishe timu hiyo inacheza soka ya kushambulia zaidi na kwa sababu hiyo wameteua mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United.
  Allardyce alisema: "Teddy alikuwa ana nia ya kuingia kwenye ukocha wakati huu, hivyo wote wazi tunafurahia kumpata katika benchi la ufundi ili kutuongezea ujuzi wake katika safu yetu ya ushambuliaji,".
  Amerudi West Ham: Teddy Sheringham anatarajiwa kujiunga btena na West Ham, klabu aliyoichezea kati ya mwaka 2004 na 2007
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TEDDY SHERINGHAM AREJEA WEST HAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top