• HABARI MPYA

  Friday, May 30, 2014

  WENGER ASAINI MKATABA MPYA ARSENAL AMBAO ATAPIGA KAZI HADI MEI 2017 KWA MSHARA MTAMU KINOMA

  KOCHA Arsene Wenger amesaini Mkataba mpya wa mshahara wa Pauni Milioni 8 kwa mwaka Arsenal, amnao utamalizika mwaka 2017. 
  Wenger alimaliza utata wote juu ya mustakabali wake kwa kukubali mkataba mpya baada ya kushinda taji la Kombe la FA mwezi guu. 
  Kulikuwa kuna wasiwasi mwalimu huyo wa Kifaransa mwenye umri wa miaka 64 angeondoka kama angeshindwa kumaliza ukame wa mataji The Gunners wa miaka tisa, lakini aliamua kubaki baada ya ushindi wa Kombe hilo dhidi ya Hull City Uwanja wa Wembley. 
  Bado nipo sana: Arsene Wenger amesaini Mkataba mpya utakaomuweka Arsenal hadi Mei mwaka 2017

  MAFANIKIO YA WENGER

  LIGI KUU ENGLAND: 1998, 2002, 2004
  KOMBE LA FA: 1998, 2002, 2003, 2005, 2014
  NGAO YA JAMII: 1998, 1999, 2002, 2004
  LIGI YA MABINGWA: Fainali mwaka 2006 wakafungwa na Barcelona)
  KOMBE KLA UEFA: Faiali mwaka 2000 wakafungwa kwa penalti na Galatasaray)
  KOMBE LA LIGI: Fainali mwaka 2007 wakafungwa na Chelsea, 2011 wakafungwa na Birmingham)
  TUZO NYINGINE:
  KOCHA WA MWAKA WA LMA: 2001-02, 2003-04
  KOCHA BORA WA MUONGO WA SHIRIKISHO LA KIMATAIFA LA TAKWIMU NA HISTORIA ZA SOKA: 2000-2010
  Kusainiwa kwa Mkataba huo unatarajiwa mwanzo wa Wenger kurejesha zama za furaha ndani ya Arsenal kwa kushinda mataji zaidi kuanzia msimu ujao. 
  Mwenyekiti wa Arsenal, Sir Chips Keswick amesema: "Tunafurahi kwamba Arsene amesaini Mkataba mpya kwa miaka mitatu zaidi. Ni mtu wa misimamo, ambaye anaishi na kuipenda Arsenal. Ameipambanu Arsenal kwa mtindo wake mzuri wa uchezaji wa soka ya kisasa duniani kote, akiendeleza mshikamano wake na wachezaji chipukizi na ana fursa ya kuongeza wachezaji wa kiwango cha juu katika klabu. Sina shaka tuna mustakabali wa kupendeza mbele yetu na yeye akiiongoza timu,".
  Mwanahisa Mkuu wa Arsenal, Stan Kroenke, kwa upande wake nays amesema: "Kudumu katika kiwango kizuri ni jambo gumu kumudu katika mchezo na ukweli ni kwamba  Arsenal imekuwa mshindani wa nafasi za juu katika soka ya England na Ulaya wakati wote wa Arsene akiwa kocha,".
  Tangu atue Arsenal akitokea  Nagoya FC ya Japan miaka 18 iliyopita, Wenger ameiongoza The Gunners kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya England na matano ya Kombe la FA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENGER ASAINI MKATABA MPYA ARSENAL AMBAO ATAPIGA KAZI HADI MEI 2017 KWA MSHARA MTAMU KINOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top