• HABARI MPYA

  Saturday, May 24, 2014

  POLISI ZENJI ILIVYOFANYWA KITU MBAYA NA EL MERREIKH USIKU WA JANA OMDURAN

  Na Rodgers Mulindwa, KHARTOUM
  POLISI ya Zanzibar imeanza vibaya michuano ya Nile Basin baada ya kufumuliwa mabao 3-0 na wenyeji El Merreikh katika mchezo wa ufunguzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Merreikh, Omduran. 
  Vigogo wa Sudan waliokuwa wanacheza kwenye uwanja wao wa nyumbani kwa mara ya kwanza baada ya miezi sita ya kuhamia Uwanja wa Khartoum kupisha ukarabati, jana waliuatwala mchezo na kuipoteza kabisa Polisi. 
  Kikosi cha Polisi Zanzibar kilichopigwa 3-0 jana Sudan

  El Merreikh, inayoundwa na mkusanyiko wa vipaji kutoka nchi mbalimbai barani, wakiwemo wachezaji kutoka Ghana, Mali, Ivory Coast, Nigeria, Burkina Faso na Ethiopia, waliwavutia mashabiki wao 44,000. 
  Walionekana bora chini ya kocha mkongwe, Martin Otto Pfister, Mjerumani mwenye umri wa miaka 76 ambaye aliikochi Saudi Arabia katika michezo wa Olimpiki, Cameroon, Togo, Ghana, Zaire, Ivory Coast, Senegal na Trinidad & Tobago.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mashood Ssali aliyesaidiwa na Lee Okello wote wa Uganda na Farhan Bogoreh wa Djibouti, mabao ya wenyeji yalifungwa na Olivier Tia Togbe dakika ya 22, Faisal Juma dakika ya 48 na Mohamed Traore kutoka Mali dakika ya 86.
  Kikosi cha Al-Merreikh kilikuwa; Eihab Mohamed, Balla Gabir, Amir Kamal/Alvi Fakou dk73, Ghandi Kassenu, Serge Pascal Wawa, Alaedin Yousif, Bassirou Bamba/Ahmed Abdallah dk42, Faisal Musa, Ramadhan Agab/Ahmed El Basha dk86, Olivier Tia Togbe na Mohamed Traore.
  Polisi; Nassir Suleiman Mzee, Juma Ali Silima, Mohamed Hassan Vuai, Mohamed Othman Mmanga, Rashid Jumanne Kavuruga/Amir Adam Amir dk85, Ismael Khamis Amour, Mohamed Seif Mohamed, Abdallah Omar Ali, Khamis Abdulrahman Hamad/Haule Innocent Haule dk70 na Sadir Ali Abdallah/Khalid Kheir Mtwana dk40.
  vuze (Burundi)
  Michuano hiyo mipya ya CECAFA ilifunguliwa mapema Saa 11.30 Uwanja wa Al Merreikh, kwa SC Victoria University ya Uganda kuifunga 1-0 Malakia ya Sudan Kusini, bao pekee la Maurishi Jjuuko dakika ya 12.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI ZENJI ILIVYOFANYWA KITU MBAYA NA EL MERREIKH USIKU WA JANA OMDURAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top