• HABARI MPYA

  Saturday, May 24, 2014

  DAVID LUIZ ATOA STETIMENTI NZITO; "NAONDOKA CHELSEA KWA MACHUNGU MAKUBWA"

  BEKI David Luiz amesema kwamba anaondoka Chelsea na 'machungu makubwa' baada ya kukamilisha vipimo vya afya na kufaulu kuhamia Paris Saint-Germain kwa dau la Pauni Milioni 50 linalomfanya awe beki ghali zaidi duniani kwa sasa. 
  Chelsea imethibitisha jana katika tovuti yake kumuuza mlinzi huyo wa Kibrazil, kabla ya Luiz kutoa taarifa inayoelezea machungu yake kwa kuondoka Stamford Bridge baada ya kupiga kazi kwa takriban miaka minne. 
  Naondoka na machungu: Luiz anayesherehekea taji la Europa League baada ya Chelsea kuifunga Benfica kwenye fainali mwaka jana, amesema anaondoka na machungu makubwa Stamford Bridge.

  "Asante Chelsea kwa miaka mitatu na nusu ya uhusiano mzuri,"amesema Luiz. "Nimetengeneza marafiki wazuri, nimeshinda mataji mengi na kumbukumbu hizo hazitaondoka kwangu. Ningependa kuwashukuru wachezaji wenzangu, viongozi wote na mashabiki wote.
  "Ninaondoka na machungu makubwa, lakini wakati huo huo ninavutiwa na changamoto mpya, ninayokwenda kukutana katika klabu kubwa kwenye mii ambao wakati wote nimekuwa nikiutamani. Ni hatua mpya, changamoto mpya na kwa pamoja tutafika. Kwaherini,"alisema.

  Thanks: Luiz posted this message on Facebook after Chelsea announced his move to France
  Shukrani: Luiz ameposti ujumbe huu katika ukurasa wake wa Facebook baada ya Chelsea kutangaza kumuuza Ufaransa

  Beki huyi mwenye umri wa miaka 27 anaconda kuwa mchezaji ghali zaidi wa nafasi ya ulinzi, akivunja rekodi za wachezaji waliosajiliwa PSG kabla yake, Marquinhos na Thiago Silva.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DAVID LUIZ ATOA STETIMENTI NZITO; "NAONDOKA CHELSEA KWA MACHUNGU MAKUBWA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top