// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); GAMONDI AONDOKA TANZANIA AKIIACHIA YANGA ‘UJUMBE MZITO’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE GAMONDI AONDOKA TANZANIA AKIIACHIA YANGA ‘UJUMBE MZITO’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, November 27, 2024

    GAMONDI AONDOKA TANZANIA AKIIACHIA YANGA ‘UJUMBE MZITO’


    ALIYEKUWA Kocha wa Yanga, Muargentina Miguel Angel Gamondi ameondoka Alfajiri ya leo kurejea kwao huku akisema ataikumbuka daima timu hiyo na anajivunia kuwa sehemu ya wana Jangwani.
    Gamondi ameposti picha akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam Alfajiri ya leo tayari kuondoka na kuambatanisha na ujumbe usemao;
    “Asanteni sana. Asante sana wananchi, kwa wachezaji wangu na kila mtu. Ninashukuru sana na ninajivunia kuwa sehemu ya Yanga kwa wakati wangu. Mtakuwa moyoni mwangu daima. Upendo mwingi,”.

    Gamondi anaondoka siku moja baada ya Yanga kucharazwa mabao 2-0 na Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa kwanza wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Ulikuwa mchezo wa kwanza Yana inacheza bila yeye na wa tatu mfululizo kupoteza pamoja na zile mbili za Ligi Kuu walizochapwa 1-0 na Azam FC na 3-1 na Tabora United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam zilizomfukuzisha Muargentina huyo.
    Mabao yaliyoizamisha Yanga jana yalifungwa na washambuliaji Adama Coulibaly wa Mali dakika ya 63 akimalizia pasi ya beki Altayeb Abdelrazig na Yasir Mozamil dakika ya 90 akimalizia pasi ya kiungo Abdel Raouf Yagoub.
    Yanga jana iliongozwa na kocha mpya, Mjerumani mwenye asili ya Bosnia and Herzegovina, Sead Ramovic aliyechukua nafasi ya Gamondi aliyefukuzwa wiki iliyopita baada ya msimu mmoja na nusu kazini.
    Gamondi ameiachia Yanga matatu ya nyumbani, Ligi Kuu, Kömbe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Ngao ya Jamii pamoja na kuifikisha timu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambako iliyolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa penalti baada ya sare za bila mabao nyumbani na ugenini.
    Mechi nyingine ya Kundi A jana, wenyeji TP Mazembe waliambulia suluhu mbele ya MC Alger Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
    Yanga watakuwa na mchezo mmoja wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC Jumamosi Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi kabla ya kusafiri kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa pili wa Kundi Ligi ya Mabingwa dhidi ya wenyeji, MC Alger Desemba 7 kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GAMONDI AONDOKA TANZANIA AKIIACHIA YANGA ‘UJUMBE MZITO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top