// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 2-1 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 2-1 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, November 28, 2024

    AZAM FC YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 2-1 CHAMAZI


    WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo Feisal Salum Abdallah dakika ya 38 na mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Alfonso Blanco Yus dakika ya 57, wakati bao pekee la Singida Black Stars limefungwa na Elvis Baranga Rupia dakika ya 62.
    Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 12, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Simba SC ambayo pia ina mchezo mmoja mkononi.
    Singida Black Stars inayofikisha mechi nne bila ushindi, leo ikifungwa mara ya pili na drop mbili - inabaki na pointi zake 24 za mechi 12 nafasi ya nne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 2-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top