• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 15, 2009

  MISS DAR MZIZIMA NI GLORY WILLIAM

  Glory akipewa zawadi na mgeni rasmi, Profesa Dusan Kondic kocha wa Yanga
  Washindi wa Miss Dar Mzizima 2009 pichani

  GLORY William (20), Juni 6, mwaka huu alifanikiwa kutwaa taji la Miss Dar Mzizima 2009 baada ya kuwabwaga wenzake 12 katika shindano lililofanyika katika Ukumbi wa Afri Centre uliopo Ilala, Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Glory alizawadiwa Dola za Marekani 400, wakati Irene Karugaba aliyeshika nafasi ya pili, alipata Dola za Marekani 300, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Pendo Lema aliyejinyakulia Dola za Marekani 200. Nafasi ya nne ilikwenda kwa Hadija Muheche na ya tano Nyamizi Mihayo ambao kila mmoja alijinyakulia Dola za Marekani 100. Warembo wote hao wamekata tiketi ya kushiriki katika kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Ilala kitakachofanyika Julai 18 katika Ukumbi wa Lamada, pia uliopo Ilala. Glory, aliyetumia lugha ya Kiingereza katika kujieleza, alijibu vizuri mno swali aliloulizwa, hali iliyoufanya umati uliokuwapo ukumbini hapo kumshangilia kwa nguvu mno. Shindano hilo ambalo mgeni rasmi alikuwa ni kocha wa mabingwa wa soka nchini, Yanga, Profesa Dusan Kondic, na kupambwa na burudani kutoka kwa bendi ya muziki wa dansi ya Diamond Musica International na wasanii wa Bongo Fleva, Pipi na Barnaba, lilifana mno.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MISS DAR MZIZIMA NI GLORY WILLIAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top