TIMU ya TRA United imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki wa kati Muivory Coast, Chamou Karaboue dakika ya 13 na kwa ushindi huo, TRA United inafikisha pointi 40 katika mchezo wa 26 na kusogea nafasi ya tano.
Hali inazidi kuwa mbaya kwa KMC FC ikiendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 kwa kubaki na pointi zake tisa za mechi 26.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment