• HABARI MPYA

    Thursday, May 08, 2014

    MICHUANO YA BEACH SOOCER YAINGIA ROBO FAINALI

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    MICHUANO ya soka ya ufukweni (beach soccer) inayoendeshwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikishirikisha vyuo mbalimbali vya Dar es Salaam imeingia hatua ya robo fainali.
    Robo fainali hiyo inayoshirikisha timu nane itachezwa Jumamosi (Mei 10 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni kuanzia saa 5 asubuhi, huku Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Taasisi ya Ustawi wa Jamii (SWI) zikicheza robo fainali ya kwanza.

    Chuo Kikuu cha Ardhi (AU) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere watcaheza robo fainali ya pili kuanzia saa 6 kamili. Saa 8 kamili itaanza robo fainali ya tatu itakayozikutanisha Taasisi ya Uhasibu (TIA) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
    Robo fainali ya mwisho itakayoanza saa 9 kamili itakuwa kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Utumishi Magogoni. Washindi watacheza nusu fainali Jumapili (Mei 11 mwaka huu) kwenye ufukwe huo huo.

    Mechi za kutafuta mshindi wa tatu, na ile ya fainali zitachezwa kwenye ufukwe huo huo wikiendi ya Mei 17 mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHUANO YA BEACH SOOCER YAINGIA ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top