Na Princess Asia, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mrisho Ngassa amesema Simba na Azam hata
wamfuate na makontena ya fedha, hatahama Jangwani.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa
Simba SC, Khalfan Ngassa amesema kwamba anataka kucheza Yanga SC hadi mwisho wa
soka yake.
Lakini nyota huyo amesema; “Naweza kuondoka Yanga SC iwapo tu
nitapata ofa ya nje ya nchi, lakini kwa sasa akili yangu ni kucheza Yanga hadi
mwisho wa soka yangu,”amesema.
![]() |
| Mimi Yanga tu; Mrisho Ngassa amesema atapenda amalizie soka yake jangwani |
Ngassa amesema alitaka kuweka rekodi ya kucheza klabu zote kubwa
nchini na anashukuru amecheza Azam FC na Simba SC, hivyo sasa hana mpango wa
kuhama Yanga SC.
“Ukiwa mchezaji mzuri, kila klabu itataka huduma yako. Naamini
hata Mbeya City wangependa kuwa na Mrisho Ngassa kwa wakati huu, lakini wakati
mwingine mtu lazima uwe na maamuzi bila kuyumbishwa na fedha,”amesema.
Mashabiki wa Yanga wananipenda sana, wakati wote nawafikiria wao,
namna gani nifanye wafurahi, huwa wananihamasisha kucheza kupita uwezo
wangu,”ameongeza Ngassa.



.png)
0 comments:
Post a Comment