TIMU ya Mamlaka ya Jiji la Kampala (KCCA) imefanikiwa kutetea
ubingwa wa Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA Super League) baada ya
kuichapa mabao 3-1 Sports Club Villa Uwanja wa KCCA eneo Lugogo mjini Kampala,
jana.
Kiungo wa zamani wa Yanga SC ya Tanzania, Steven Bengo alifunga
bao la kwanza la KCCA dakika ya 21, kabla ya beki Ronnie Kisekka kufunga la
pili dakika chache kabla ya mapumziko.
![]() |
| Mabingwa; KCC wakisherehekea na taji lao |
William Wadri akafunga bao la tatu kabla ya Kiseeka kujifunga
kuipatia SC Villa bao la kufutia machozi.
Kwa ushindi huo, KCCA imetimiza pointi 60 kutoka mechi 30, moja
zaidi ya SC Victoria University
inayoshika nafasi ya pili.
Hilo ni taji la 10 kwa KCC la Ligi Kuu ya Uganda na sasa mwakani
watacheza tena michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati SC Victoria
University itaiwakilisha Uganda kwenye Kombe la shirikisho.
Kocha wa KCCA,
George Nsimbe amesema atahakikisha anatimiza malengo ya kutwaa mataji mawili
kwa kutwaa pia na Kombe la Ligi, michuano ambayo wametinga fainali na
watakutana na SC Victoria University.
Wakati KCC wametetea ubingwa wao wa Uganda, nchini Tanzania waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC wamevuliwa taji na Azam FC.



.png)
0 comments:
Post a Comment