• HABARI MPYA

    Sunday, June 14, 2026

    BRAZIL NA MOROCCO MBAVU SAWA, ZATOA SARE 1-1 KOMBE LA DUNIA


    TIMU ya Brazil imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Morocco katika mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Dunia usiku wa Jumamosi Uwanja wa MetLife mjini East Rutherford, New Jersey Jijini New York, Marekani. 
    Kiungo wa PSV Eindhoven ya Uholanzi, Ismael Saibari mzaliwa wa Hispania alianza kuwafungia ‘mabingw awa mezani’ wa Afrika, Morocco dakika ya 21, kabla ya mshambuliaji wa Real Madrid, Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior kuisawazishia Brazil dakika ya 32.
    Mechi nyingine ya Kundin C Kombe la Dunia inaendelea muda huu baina ya Haiti na Scotland Uwanja wa Gillette mjini Foxborough, Norfolk County, Massachusetts, Marekani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BRAZIL NA MOROCCO MBAVU SAWA, ZATOA SARE 1-1 KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top