MTAALAMU Louis Van Gaal amesema angependa kuwa mocha mpya wa Manchester United.
Mwalimu huyo wa Kiholanzi mwenye umri wa miaka 62, anatarajiwa kutambulishwa rasmi kama kocha mpya wa timu ya Old Trafford wiki ijayo, mara klabu hiyo itakapoafiki muundowa bench lake la ufundi.
Akizungumza nchini Uholanzi, mocha huyo wa timu ya taiga ya Uholanzi alisema bado anazungumza na klabu nyingine, lakini angependa kuwa mocha wa United.
Karibu anakuja? Louis van Gaal ameonyesha kuwa tayari kwa kibarua Manchester United, kwa kusema angefurahi kujiunga nayo

Makocha wapya United: Van Gaal akiwa na Wasaidizi wake, Patrick Kluivert (katikati) na Frans Hoek katika mazoezi ya timu ya taiga ya Uholanzi
"Ningependa kuwa kocha (United),’ alisema Van Gaal. "Kwa kila mocha anayepata kazi ni changamoto nzuri.
"Natumai nitakuwa mimi, lakini mnatakiwa kusubiri na kuona. Kuna klabu zaidi zinanitaka. Nina uteuzi zaidi,"alisema na kuongeza.
"Tupo katika mchakato na kila mtu anatakiwa kusubiri chaguo langu kutoka klabu hizo. "Lakini United ni klabu kubwa duniani,"



.png)
0 comments:
Post a Comment