MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo alilazimika kutoka nje baada ya dakika name tu Real Madrid ikitoa safe ya 1-1 na Real Valladolid kutokana na maumivu ya nyama za paja.
Nyota huyo wa Real Madrid alipigwa picha akiwa ameshika mguu wake wa kushoto huku akizungumza na mocha wake, Carlo Ancelotti wakati wa mazoezi juzi.
Pamoja na hayo, Real ikaamu kumtumia katika mechi ya jana, zikiwa zimebaki siku 17 kabla ya Real kucheza na Atletico Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako itakutana na Atletico Madrid.
Mchezaji mwenzake Ronaldo, Gareth Bale mapema aliondolewa kwenye mchezo huo kwa sababu ya majeruhi pia.
Ronaldo alitoka dakika ya nane Uwanja wa Jose Zorilla bila ya kuonyesha dalili yoyote ya maumivu, muds mfupi baada ya kukimbia na mpira dhidi ya wachezaji wa timu pinzani na kumalizia kwa kukabiliana na mabeki wa timu hiyo.
Real Madrid ilipata boa la kuongoza kupitia kwa beki Sergio Ramos aliyefunga kwa mpira wa adhabu, lakini Humberto Osorio akawasawazishia wenyeji mwishoni mwa mchezo.
Shakani: Ronaldo akiwa ameketi uwanjani baada ya kukwatuliwa katika mchezo wa jana usiku
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ureno hive karibuni alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya goti na misuli katika mguu wake wa kushoto, lakini alirejea uwanjani katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa wakiitoa Bayern Munich.
Ronaldo hadi sass amefunga mabao 50 msimu huh kwenye mashindano yote, yakiwemo ya kwenye ligi 31 yanayomfanya aongoze kwa mabao La Liga.



.png)
0 comments:
Post a Comment