• HABARI MPYA

    Thursday, May 08, 2014

    UJERUMANI YATAJA KIKOSI CHA KOMBE LA DUNIA, OZIL...

    WACHEZAJI watatu wa Arsenal, Lukas Podolski, Mesut Ozil na Per Mertesacker wote wamejumuishwa katika kikosi cha Ujerumani kitakachoingia kambini kujiandaa na Fainali za Kombe la Dunia.
    Mshambuliaji wa Chelsea, Andre Schurrle pia atakwenda Brazil mwezi ujao baada ya kujumishwa kwenye kikosi cha Joachim Low.
    Kiungo wa Real Madrid, Sami Khedira pia ameitwa, licha ya kwamba hajacheza tang Novemba mwaka jana sababu ya majeruhi.
    Amepata kiatu, lakini si Ujerumani: Mesut Ozil, pichani akiwa ameshika kiatu wakati wa promosheni ya hisani, naye pia atakwenda Kombe la Dunia

    Kikosi kamili cha Ujerumani ni makipa: Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller (Borussia Dortmund) na and Ron-Robert Zieler (Hannover), mabeki; Erik Durm (Borussia Dortmund), Jerome Boateng (Bayern Munich), Kevin Grosskreutz (Borussia Dortmund), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Marcell Jansen (Hamburg), Philipp Lahm (Bayern Munich), Per Mertesacker (Arsenal), Shkodran Mustafi (Sampdoria) na Marcel Schmelzer (Borussia Dortmund). 
    Viungo ni Lars Bender (Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Schalke), Matthias Ginter (Freiburg), Leon Goretzka (Schalke), Mario Gotze (Bayern Munich), Andre Hahn (Augsburg), Sami Khedira (Real Madrid), Toni Kroos (Bayern Munich), Max Meyer (Schalke), Thomas Müller (Bayern Munich), Mesut Ozil (Arsenal) na Marco Reus (Borussia Dortmund) wakati washambuliaji ni Lukas Podolski (Arsenal), Andre Schurrle (Chelsea), Miroslav Klose (Lazio) na Kevin Volland (Hoffenheim).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UJERUMANI YATAJA KIKOSI CHA KOMBE LA DUNIA, OZIL... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top