MANCHESTER City imejisogeza karibu kabisa na ubingwa wa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa usiku huh kwenye Uwanja wa Etihad, Manchester England.
Shukrani kwake Edin Dzeko aliyefunga mabao mawili katika dakika za 64 na 72 wakati boa lingine la City lilifungwa na Yaya Toure dakika ya tatu ya muds wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida za mchezo.
City sasa inatimiza point 83 baada ya kucheza mechi 37 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England, ikihitaji tu ushindi katika mechi ya mwisho Mei 11 kujihakikishia ubingwa.
Liverpool yenye pointi 81 za mechi 37 pia inashika nafasi ya pili, wakati Chelsea yenye pointi 79 za mechi 37 nayo ni ya tatau. Msimu wa Ligi Kuu ya England utahitimihswa Mei 11 kwa mechi kati ya Cardiff City na Chelsea, Fulham na Crystal Palace, Hull City na Everton, Liverpool na Newcastle United, Manchester City na West Ham United, Norwich City na Arsenal, Southampton na Manchester United, Sunderland na Swansea City, Tottenham Hotspur na Aston Villa na West Bromwich na Stoke City.



.png)
0 comments:
Post a Comment