// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WINGA ALIYEMTESA KAPOMBE JANA AOMBA DOLA 1,000 TU ASAINI LIGI KUU BARA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WINGA ALIYEMTESA KAPOMBE JANA AOMBA DOLA 1,000 TU ASAINI LIGI KUU BARA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, May 19, 2014

    WINGA ALIYEMTESA KAPOMBE JANA AOMBA DOLA 1,000 TU ASAINI LIGI KUU BARA

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    WINGA aliyekuwa akimsumbua Shomary Kapombe upande wa kushoto wa Uwanja jana, Kudakwashe Mahachi ameomba mshahara wa dola za Kimareakni 1,000 kwa klabu yoyote ya Tanzania itakayotaka kumsajili pamoja na ada ya kusaini.
    Winga huyo wa chipukizi wa Zimbabwe amesema kwa kuwa yeye bado kijana mdogo hataki mshahara mkubwa kucheza Tanzania, bali dola 1,000 kwa mwezi itamtosha.
    Dola 1,000 unabeba kifaa; Winga wa Zimbabwe, Kudakwashe Mahachi ameomba mshahara wa dola 1,000 tu acheze Tanzania
    Mahachi akishangilia moja ya mabao aliyowahi kuifungia Zimbabwe

    “Niko tayari kujiunga na klabu yoyote ya Tanzania kwa mshahara wa doa 1,000 tu, naondoka kurudi Zimbabwe ila timu ambayo imevutiwa na mimi inaweza kunifuata tumalizane,”alisema mchezaji huyo wa Chicken Inn F.C.
    Bao pekee la mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ jana dakika ya 13 akimalizia krosi ya Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC liliipa Taifa Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya Zimbabwe katika mchezo huo.
    Ushindi huo mwembamba unaipa Taifa Stars mzigo wa kwenda kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu kwenye mchezo wa marudiano Juni 1, ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo kuwania nafasi ya kuingia kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2015 nchini Morocco.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WINGA ALIYEMTESA KAPOMBE JANA AOMBA DOLA 1,000 TU ASAINI LIGI KUU BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top