// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIPA ZIMBABWE ATAKA TIMU DAR, LAKINI AOMBA MSHAHARA HUO HAKUNA YEYOTE ANAYELIPWA LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIPA ZIMBABWE ATAKA TIMU DAR, LAKINI AOMBA MSHAHARA HUO HAKUNA YEYOTE ANAYELIPWA LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, May 19, 2014

    KIPA ZIMBABWE ATAKA TIMU DAR, LAKINI AOMBA MSHAHARA HUO HAKUNA YEYOTE ANAYELIPWA LIGI KUU

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    KIPA wa Zimbabwe, George Chigova amesema kama kuna timu ya Tanzania inamtaka, basi iwe tayari kumlipa mshahara wa dola za Kimarekani 15,000 kwa mwezi.
    Akizungumza jana katika hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es Salaam ambako timu hiyo ilifikia, kipa huyo aliyedaka vizuri na kuizuia Tanzania kuondoka na ushindi mnene alisema yuko tayari kucheza Tanzania.
    Mlinda mlango huyo wa klabu ya Dynamos F.C. ya Zimbabwe mwenye umri wa miaka 23 amesema kwamba ndoto zake ni kucheza soka ya kulipwa Ulaya, ila atakuwa tayari kuondokea hata Tanzania.
    Geroge Chigova ameomba mshara wa dola 15, 000 acheze Tanzania


    “Wote tunacheza Afrika kutafuta nafasi za kwenda Ulaya, kama ipo klabu Tanzania inacheza michuano ya Afrika itataka kunisajili, nipo tayari ila kwa mshahara wa dola 15,000,”alisema.
    Kipa huyo alifungwa bao moja tu na mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ jana dakika ya 13 akimalizia krosi ya Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC.
    Ushindi huo mwembamba unaipa Taifa Stars mzigo wa kwenda kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu kwenye mchezo wa marudiano Juni 1, ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo kuwania nafasi ya kuingia kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2015 nchini Morocco.  
    Kwa sasa, mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi nchini ni Emmanuel Okwi wa Yanga SC  4,000 kwa mwezi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPA ZIMBABWE ATAKA TIMU DAR, LAKINI AOMBA MSHAHARA HUO HAKUNA YEYOTE ANAYELIPWA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top