• HABARI MPYA

        Sunday, May 18, 2014

        ASEC WAANZA NA SARE YA UGENINI MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

        VIGOGO wa Ivory Coast, ASEC Mimosas wamelazimisha sare ya ugenini ya kufungana bao 1-1 na wenyeji AS Real Bamako kwenye Uwanja wa Modibo Keita, katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika.
        Baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika bila timu hizo kufungana, timu kutoka Jiji la Abidjan ilipata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo mkabaji Mcameroon, Michel Mvondo.
        Michel Mvondo aliifungia bao la kuongoza ASEC

        Lakini zikiwa zimesalia dakika nne mchezo kumalizika, timu ya Mali ilipata bao la kusawazisha kupitia kwa Moussa Kone aliyefunga kwa penalti.
        Timu nyingine katika kundi hilo ni AC Leopards ya Kongo na Coton Sport ya Cameroon ambazo zitamenyana kesho.
        Wikiendi ijayo, ASEC Mimosas itakuwa mwenyeji wa AC Leopards wakati AS Real Bamako itasafiri hadi Garoua kuifuata Coton Sport.

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: ASEC WAANZA NA SARE YA UGENINI MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry