MABAO ya Arjen Robben na Thomas Mueller katika dakika za nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida, yametosha kuipa Bayern Munich ushindi wa 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund na kutwaa Kombe la Ujerumani usiku huu, hilo likiwa taji la pili kwa timu hiyo katika msimu wa kwanza wa kocha Pep Guardiola kazini.
Robben alifunga dakika ya 107 baada ya kuunganisha krosi ya Jerome Boateng aliyemtoka Roman Weidenfellert kabla ya Mueller kumzunguka Weidenfeller kufunga la pili dakika za majeruhi.
Robert Lewandowksi aliichezea Dortmund mechi yake ya mwisho kabla ya kuhamia Bayern Munich Julai 1, mwaka huu na usiku huu aliwekewa ulinzi mkali na Boateng na Dante.
Kifaa; Arjen Robben akisherehekea baada ya kufunga bao la kwanza
Kitaalamu: Arjen Robben akiifungia Bayern Munich bao la kwanza dhidi ya Borussia Dortmund
0 comments:
Post a Comment