KOCHA wa Cameroon, Volker Finke amewajumuisha mshambuliaji mkongwe Samuel Eto na chipukizi Vincent Aboubakar katika kikosi chake cha awali cha wachezaji 28 kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Nchini Tanzania Eto'o ni maarufu kwa jina la shemeji, baada ya kukutwa na kashfa ya kutoka na binti wa Dar es Salaam wakati Cameroon imekuja kwa ajili ya mechi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010.
Kikosi cha Finke kimewabeba pia beki wa Tottenham, Benoit Assou-Ekotto, kiungo wa Barcelona, Alex Song na nyota wa Rennes, Jean Makoun.
Cameroon ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufika Robo Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1990 nchini Italia, lakini tang halo imekuwa haifanyi vizuri. Cameroon ilifungwa mechi zake taut za kundi lake nchini Afrika Kusini miaka mine iliyopita.
Mshambuliaji kinda wa miaka 22, Aboubakar amekuwa na msimu mzuri klabu ya Lorient nchini Ufaransa, wakati Nahodha Eto'o anajiandaa kucheza fainali zake za nne za Kombe la Dunia.
Kikosi kamili ni makipa: Charles Itandje (Konyaspor/Uturuki), Ndy Assembe (Guingamp/Ufaransa), Sammy Ndjock (Fetihespor/Uturuki), Loic Feudjou (Coton Sport), mabeki; Allan Nyom (Granada/Hispania), Dany Nounkeu (Besiktas/Uturuki), Cedric Djeugoue (Coton Sport), Aurelien Chedjou (Galatasaray/Uturuki), Nicolas Nkoulou (Marseille/Ufaransa), Armel Kana-Biyik (Rennes/Ufaransa), Henri Bedimo (Lyon/Ufaransa), Benoit Assou-Ekotto (QPR/England) na Gaetang Bong (Olympiakos/Ugiriki).
Viungo; Eyong Enoh (Antalyaspor/Uturuki), Jean II Makoun (Rennes/Ufaransa), Joel Matip (Schalke 04/Ujerumani), Stephane Mbia (Sevilla/Hispania), Landry Nguemo (Bordeaux/Ufaransa), Alexandre Song (Barcelona/Hispania), Cedric Loe (Osasuna/Hispania) na Edgar Sally (Lens/Ufaransa).
Washambuliaji; Samuel Eto'o (Chelsea/England), Eric Choupo Moting (Mainz/Ujerumani), Benjamin Moukandjo (Nancy/Ufaransa), Vincent Aboubakar (Lorient/Ufaransa), Achille Webo (Fenerbahce/Uturuki), Mohamadou Idrissou (Kaiserslautern/Ujerumani), Fabrice Olinga (Zulte-Waregem/Ubelgiji).
Simba Wasiofungika wapo Kundi A pamoja na wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.



.png)
0 comments:
Post a Comment