Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KLABU ya Azam FC imeingia Mkataba wa miaka mitatu na beki chipukizi wa kati, Abdallah Kheri Salum wa klabu ya Zimamoto ya Zanzibar.
Beki huyo anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia, kwa sasa yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Beki huyo mwenye kipaji aliendeleza ada yake kwa kucheza vizuri Jumapili Ngorongoro ikimenyana na Nigeria, Flying Eagles licha ya kufungwa mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wasaka vipaji wa Azam FC baada ya kumfuatilia kwa muda mrefu mchezaji huyo tangu anacheza visiwani Zanzibar waliridhishwa naye na kumuingiza kwenye mipango yao ya muda mrefu.
“Ni mchezaji mdogo mwenye kipaji, ambaye wasaka vipaji wetu wamejiridhisha atakuwa msaada kwa timu yetu baadaye, hivyo tumeamua kumpa Mkataba wa miaka mitatu,”amesema Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa.
Kwa upande wake, mchezaji mwenyewe amesema amefurahi kujiunga na Azam FC, kwa kuwa ni timu kubwa na anaamini ni fursa nzuri kwake kuendeleza kipaji chake. “Ni mabingwa wa Tanzania (Bara), ni timu kubwa na bora ambayo naamini ni bahati kwangu kujiunga nayo, ninaamini nitaendeleza kipaji changu na kutimiza ndoto za kuwa mchezaji bora baadaye,”amesema Kheri.
Huyo anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Azam baada ya kumaliza msimu na taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Wengine waliosajiliwa Azam FC ni kiungo Frank Domayo, mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu kutoka Yanga SC na mshambuliaji Ismaila Diara kutoka Mali.
Azam FC pia ipo katika mpango wa kumsajili kiraka, Shomary Kapombe wa AS Cannes ya Ufaransa, ambaye amegoma kurejea kujiunga na klabu hiyo aliyojiunga nayo akitokea Simba SC katikati ya mwaka jana.
Tayari Kapombe anayeweza kucheza nafasi zote za ulinzi na kiungo amekwishaanza kufanya mazoezi na Azam FC tangu Machi mwaka huu, baada ya kugoma kurejea Ufaransa Novemba mwaka jana alipokuja kwa ruhusa ya kuichezea timu ya taifa, Taifa Stars.

![]() |
| Abdallah Salum Kheri ametua Azam FC |

.png)
0 comments:
Post a Comment