Na Princess Asia, Kinshasa
AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeanza vyema hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga mabao 2-1 Zamalek ya Misri katika mchezo wa Kundi A mjini Kinshasa jana.
Ni wiki moja tangu baada ya janga kutokea kwenye Uwanja wao lililosababisha vifo vya mashabiki zaidi ya 15, lakini Vita walisahau yote na kuibuka na ushindi dhidi ya wazoefu 'White Knights’.
Tukio la maafa lilitokea baada ya mashabiki wa Vita kuvamia uwanjani kufuatia kipigo cha bao 1-0 nyumbani katika mchezo wa Ligi Kuu ya DRC kutoka kwa wapinzani wao, TP Mazembe.
Klabu hiyo ya DRC ilipata bao la kwanza dakika ya 19 kupitia kwa Ndombe Mubele ambalo lilidumu hadi dakika za mwishoni.
Lakini Moamen Zakaria wa Zamalek akaifungia timu yake bao la kusawazisha dakika ya 80, kala ya Vita kupata bao la ushindi dakika mbili baadaye kupitia kwa Emmanuel Ngudikana.
Wiki ijayo, Zamalek itakuwa mwenyeji wa Al Hilal wakati TP Mazembe itaikaribisha Vita mjini Lubumbashi. Juzi, Mazembe ilifungwa 1-0 na El Hilal katika mchezo mwingine wa kundi hilo mjini Khartoum.

0 comments:
Post a Comment