• HABARI MPYA

    Wednesday, May 21, 2014

    DIEGO COSTA ATUA SERBIA KUTIBIWA NA MGANGA WA KIENYEJI APONE HARAKA ILI ACHEZE FAILANI JUMAMOSI LIGI YA MABINGWA

    MSHAMBULIAJI Diego Costa amesafiri kwenda Belgrade kumuona mganga wa kienyeji Marijana Kovacevic maarufu kama 'Dokta Miujiza' kuhakikisha anakuwa fiti tayari kucheza mechi kubwa zaidi maishani mwake.
    Mserbia huyo anatumia placenta kuwasaidia wachezaji kupona haraka matatizo ya misuli na Jumamosi Costa anataka kuichezea Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Costa anasumbuliwa na maumivu ya nyama, aliyoyapata katika mechi ya mwisho ya La Liga dhidi ya Barcelona, ambayo Atletico ilitoa sare ya 1-1 na kutwaa taji la Ligi hiyo Kuu Hispania. 
    Tiba za asili: Diego Costa akiwa Belgrade, ambako anakutana na 'mganga placenta' ili apone haraka

    Maumivu ya aina hiyo kwa kawaida yanawaweka wachezaji née ya Uwanja kwa siku zisizopungua 15, ambayo itamfanya aukose mchezo wa Lisbon iwapo tiba hiyo ya asili haitafanya kazi.
    Costa ataungana tena na Atletico Madrid leo akitokea Serbia. Kovacevic amewatibu nyota kadhaa wa Ligi Kuu England halo kabla, akiwemo mshambuliaji Robin van Persie alipokuwa Arsenal na kiuno wa Chelsea, Frank Lampard.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DIEGO COSTA ATUA SERBIA KUTIBIWA NA MGANGA WA KIENYEJI APONE HARAKA ILI ACHEZE FAILANI JUMAMOSI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top