// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHUJI AJIFUA KINOMA! SWALI, ATAIBUKIA TIMU GANI MSIMU UJAO? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHUJI AJIFUA KINOMA! SWALI, ATAIBUKIA TIMU GANI MSIMU UJAO? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, May 19, 2014

    CHUJI AJIFUA KINOMA! SWALI, ATAIBUKIA TIMU GANI MSIMU UJAO?

    Na Dina Ismail, Dar es Salaam
    KIUNGO Athumani Iddi ‘Chuji’ ameziba masikio juu ya yote yanayosemwa juu yake na kuamua kujifua vikali akijiandaa na msimu ujao.
    Kiungo huyo amepitia msimu mbaya uliopita chini ya makocha wapya wa timu hiyo, Mholanzi Hans van der Pluijm na msaidizi wake, Mzalendo Charles Boniface Mkwasa walioanza kazi Yanga Januari mwaka huu.
    Makocha hao waliorithi mikoba ya Mholanzi mwingine, Ernie Brandts aliyekuwa akisaidiwa na mzalendo Freddy Felix Minziro hawakuweza kuiva chungu kimoja na Chuji kiasi cha kumuondoa taratibu katika kikosi cha kwanza.
    Anakula nondo; Athumani Iddy Chuji akijifua gym leo baada ya kumaliza kufukuza upepo ufukwe wa Coco Beach. Jioni anahamia uwanjani kuukanyaga mpira

    Makocha hao walimuondoa kabisa kambini Chuji kuelekea mechi tatu za mwisho za Ligi Kuu na inasemakana baada ya msimu wakamuweka katika orodha ya wachezaji wa kutemwa.
    Pamoja na yote, Chuji kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa amekuwa akifanya mazoezi mara tatu kwa siku, akianzia ufukweni kukimbia asubuhi, mchana gym na jioni kucheza mpira ili kujiweka fiti.
    Bado haijajulikana Chuji ataibukia timu gani msimu ujao, kwani kwa Yanga SC amekwishamaliza Mkataba wake- ingawa tetesi zinasema atarejea Simba SC, timu iliyomleta Dar es Salaam kikazi kwa mara ya kwanza mwaka 2005 akitokea Polisi ya Dodoma kabla ya kuhamia Yanga SC mwaka 2007. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHUJI AJIFUA KINOMA! SWALI, ATAIBUKIA TIMU GANI MSIMU UJAO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top