TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na mshambuliaji raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malanga Horso Mwaku dakika ya 24 na kiungo wa ulinzi, Emmanuel Kwame Keyekeh raia wa Ghana dakika ya 75, wakati bao pekee la JKT Tanzania limefungwa na mshambuliaji mzawa, Valentino Mashaka Kusengama dakika ya 81.
Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 44, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 38 nafasi ya sita ikizdiwa pointi mbili na TRA United baada ya timu hizo zote kucheza mechi 26 kwenye ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment