TIMU ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Adili Buha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 36 na kwa ushindi huo, ‘Koma Kumwanya’ wanafikisha pointi 25, ingawa wanabaki nafasi ya 14 wakizidiwa pointi mbili na Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya 12 kwenye ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment