Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeifunga bao 1-0 Zimbabwe katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2005 nchini Morocco, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa
Joseph Odartei Lamptey aliyesaidiwa na Malid Alidu Salifu na David Laryea wote wa Ghana, hadi mapumziko Taifa Stars walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 13 akiunganisha kwa guu la kushoto krosi maridadi ya mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwwengu.
Kocha wa Tanzania, Mholanzi Mart Nooij alisema baada ya mchezo huo kwamba vijana wake wamecheza vizuri, lakini wangeweza kupata mabao zaidi kama wangetumia vizuri nafasi walizotengeneza.
Kwa upande wake, kocha mzalendo wa Zimbabwe, Ian Gorowa alisema vijana walicheza vizuri, lakini walikosa bahati ya kupata mabao licha ya kutengeneza nafasi zaidi ya tatu nzuri,
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo/Amri Kiemba dk71, Mrisho Ngassa/Haroun Chanongo dk77, Mwinyi Kazimoto, John Bocco/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk85, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Zimbabwe; George Chigova, Partson Jaure, Danny Phiri, Hardlife Zvirekwi, Stephen Alimenda, Rendai Ndoro, Milton Ncube, Kudakwashe Mahachi, Cuthbert Malajila, Peter Moyo na Eric Chipeta.
Katika mechi nyingine jana, mabao mawili ya Frank ‘Gabadinho’ Mhango yaliipa Malawi ‘The Flames’ ushindi wa 2-0 dhidi ya Chad Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Sao Tome e Principe ilifungwa 2-0 nyumbani na Benin, Namibia iliilaza 1-0 Kongo na Mauritania iliibwaga 1-0 Equatorial Guinea.
Mechi nyingine za zilizotarajiwa kuchezwa ni kati ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Guinea Bissau, Swaziland na Sierra Leone, Msumbiji na Sudan Kusini, Madagascar na Uganda, Burundi na Botswana, Liberia na Lesotho, Kenya na Comoro na Libya vs Rwanda.
Mechi za marudiano zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya Mei 30 na washindi wataingia kwenye hatua ya mwisho ya mchujo ili kuwania kupangwa kwenye makundi tayari kwa mbio rasmi za Morocco 2015.

![]() |
Wachezaji wa Taifa Stars, Frank Domayo na Thomas Ulimwengu wakimkimbikia John Bocco kumpongeza baada ya kuifungia timu hiyo bao pekee dhidi ya Zimbabwe |
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 13 akiunganisha kwa guu la kushoto krosi maridadi ya mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwwengu.
Kocha wa Tanzania, Mholanzi Mart Nooij alisema baada ya mchezo huo kwamba vijana wake wamecheza vizuri, lakini wangeweza kupata mabao zaidi kama wangetumia vizuri nafasi walizotengeneza.
![]() |
Mbwana Samatta wa Tanzania akimtoka eki wa Zimbabwe |
![]() |
Mrisho Ngassa wa Tanzania akimtoka kiungo wa Zimbabwe |
![]() |
Thomas Ulimwengu wa Tanzania akimtoka beki wa Zimbabwe |
Kwa upande wake, kocha mzalendo wa Zimbabwe, Ian Gorowa alisema vijana walicheza vizuri, lakini walikosa bahati ya kupata mabao licha ya kutengeneza nafasi zaidi ya tatu nzuri,
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo/Amri Kiemba dk71, Mrisho Ngassa/Haroun Chanongo dk77, Mwinyi Kazimoto, John Bocco/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk85, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Zimbabwe; George Chigova, Partson Jaure, Danny Phiri, Hardlife Zvirekwi, Stephen Alimenda, Rendai Ndoro, Milton Ncube, Kudakwashe Mahachi, Cuthbert Malajila, Peter Moyo na Eric Chipeta.
Katika mechi nyingine jana, mabao mawili ya Frank ‘Gabadinho’ Mhango yaliipa Malawi ‘The Flames’ ushindi wa 2-0 dhidi ya Chad Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Sao Tome e Principe ilifungwa 2-0 nyumbani na Benin, Namibia iliilaza 1-0 Kongo na Mauritania iliibwaga 1-0 Equatorial Guinea.
Mechi nyingine za zilizotarajiwa kuchezwa ni kati ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Guinea Bissau, Swaziland na Sierra Leone, Msumbiji na Sudan Kusini, Madagascar na Uganda, Burundi na Botswana, Liberia na Lesotho, Kenya na Comoro na Libya vs Rwanda.
Mechi za marudiano zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya Mei 30 na washindi wataingia kwenye hatua ya mwisho ya mchujo ili kuwania kupangwa kwenye makundi tayari kwa mbio rasmi za Morocco 2015.
0 comments:
Post a Comment