MCHEZAJI anayetakiwa na Manchester United, William Carvalho ameorodheshwa katika kikosi cha awali cha Ureno cha wachezaji 30 kwa ajili ya Kombe la Dunia sambamba na Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo.
Kiungo huyo wa Sporting, ambaye anaweza kutua Old Trafford msimu ujao kama United wataendelea na nia ya kumsajili, aliichezea Ureno kwa mara ya kwanza katika mechi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya Brazil dhidi ya Sweden Novemba mwaka jana.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atakuwa pamoja kwenye kikosi hicho na mchezaji wa Mashetani Wekundu hao, Luis Nani.
Kama kawaida: Cristiano Ronaldo ataiongoza Ureno katika Kombe la Dunia
Ameteuliwa: William Carvalho (kushoto) anayetakiwa na Man United ameitwa kikosi cha Ureno
KIKOSI CHA AWALI CHA URENO HIKI HAPA;
MAKIPA: Anthony Lopes (Lyon), Beto (Sevilla), Eduardo (Braga), Rui Patricio (Sporting Lisbon)
MABEKI: Andre Almeida (Benfica), Antunes (Malaga), Bruno Alves (Fenerbahce), Fabio Coentrao (Real Madrid), Joao Pereira (Valencia), Neto (Zenit), Pepe (Real Madrid), Ricardo Costa (Valencia), Rolando (Inter Milan)
VIUNGO: Andre Gomes (Benfica), Joao Mario (Vitoria), Joao Moutinho (Monaco), Miguel Veloso (Dynamo Kiev), Raul Meireles (Fenerbahce), Ruben Amorim (Benfica), William Carvalho (Sporting Lisbon)
WASHAMBULIAJI: Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Eder (Braga), Helder Postiga (Lazio), Hugo Almeida (Besiktas), Ivan Cavaleiro (Benfica), Nani (Manchester United), Rafa (Braga), Ricardo Quaresma (Porto), Varela (Porto), Vieirinha (Wolfsburg).
0 comments:
Post a Comment