SIMBA SC wamewatangulia mahasimu wao, Yanga SC kuanza mchakato wa uchaguzi baada ya viongozi wa sasa kumaliza muda wao.
Jumapili na Jumatatu mitaa ya Kariakoo ilifungwa kwa muda kupisha maandamano ya wanachama wawili maarufu wa klabu hiyo waliokwenda kuchukua fomu za kugombea uongozi.
Hao ni Evans Elieza Aveva na Michael Richard Wambura waliochukua fomu za kugombea Urais.
Aveva alianza Jumapili akisindikizwa na mamia ya wanachama hadi makao makuu ya klabu Mtaa wa Msimbazi na Jumatatu Wambura naye akasindikizwa na umati kwenda kuchukua fomu.
Kitu kimoja niligundua, baadhi ya sura zilizokuwapo kwenye maandamano ya Aveva Jumapili zilijirudia pia katika maandamano ya Wambura Jumatatu.
Si kitu, labda wagombea hao waliteua watu wa kuwatafutia watu wa kusindikiza misafara yao na kwa bahati mbaya kuna watu walikula dili za pande zote mbili.
Lakini hakuna shaka wote waliowasindikiza vigogo hao kwenda kuchukua fomu ni wanachama wa Simba SC, ambao mwisho wa siku watapiga kura kuchagua viongozi.
Mustakabali wa klabu upo katika uchaguzi, unapochagua viongozi bora bila shinikizo la ushawishi wa aina yoyote kutoka kwa mtu yeyote, maana yake unaitengenezea mazingira klabu yako pia iwe bora.
Lakini iwapo utajali bakshishi kama kigezo cha kutoa kura yako kwa mgombea, amini klabu ikiangukia mikononi mwa kiongozi bomu, sababu itakuwa kura yako.
Vurugu zitakazofuatia baada ya mambo kwenda mrama chini ya kiongozi mbovu uliyemchagua kwa kuwa alikupa bakhshishi hazitasaidia kwa maana katiba za kisasa imara na madhubuti zitawalinda viongozi halali waliochaguliwa.
Tumeona katika utawala huu unaomaliza muda wake Simba SC, watu walichoka muda mrefu na uongozi wa Alhaj Ismail Aden Rage, lakini pamoja na hila zote walizofanya wameshindwa kumng’oa madarakani hadi anamaliza muda wake- kwa sababu katiba ilimlinda.
Mwanachama wa Simba SC anapaswa kutambua kwamba, siku moja tu ya kupiga kura kuchagua viongozi itarudi baada ya miaka minne mingine- ina maana kosa moja tu ni maumivu ya masika nne.
Sidhani kama wanachama wako tayari kuendelea kuona Yanga SC na Azam FC wanaendelea kupokezana ubingwa wa Ligi Kuu na kubadilishana tiketi za kucheza michuano ya Afrika.
Sidhani kama wanachama wa Simba SC wako tayari kuendelea kuwa klabu ya nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya Azam, Yanga na Mbeya City.
Naamini, kuyumba kwa klabu hiyo katika miaka minne iliyopita limekuwa fundisho tosha kwao na hawatakuwa tayari kurudia makosa.
Naamini sasa wana Simba SC wanajua umuhimu wa kumtathmini mgombea bila kumuangalia sura, ili kujua atafaa kuwaongoza kwa mafanikio au la.
Naamini sasa wanachama wa Simba SC watakuwa jasiri wa kutojali chochote zaidi ya kuchagua kiongozi ambaye wana imani naye na ambaye wanamjua fika, wanajua ana sapoti kubwa ya wadau akiingia madarakani ili kuweza kuiletea mafanikio klabu.
Hiyo michezo ya kuigiza maandamano bora iishie kwenye zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu, siku ya kupiga haihitaji maigizo.
Hiyo ni siku moja muhimu, inayohitaji umakini wa hali ya juu na busara ya maamuzi kwa maslahi ya klabu. Alamsiki.

.png)
0 comments:
Post a Comment