Na Zaituni Kibwana, Dar es Salaam
Julio aliyeingia kwa mbwembwe kwenye makao makuu ya klabu hiyo alichukua fomu ya kuwania nafasi ya Makamu wa Rais.
UCHAGUZI mkuu wa klabu ya Simba umepamba moto kufuatia wagombea mbalimbali kurejesha fomu kwa mbwembwe akiwemo Michael Wambura anawania nafasi ya Rais.
Wambura ambaye ni katibu mkuu wa zamani wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) zamani (FAT) amerudisha fomu hizo akisindikizwa na wanachama mbalimbali akiwemo kocha wa zamani wa timu hiyo Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
![]() |
Goffrey Nyange 'Kaburu' naye amerejesha fomu leo |
![]() |
Mehdi Burhan Mlanzi naye amerejesha fomu leo |
![]() |
Wambura kulia akikabidhi fomu leo kwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi, Khalid Kamguna |
Licha ya kuingia kwa mbwembwe na kuteka makao makuu ya klabu hiyo aliwasilisha fomu hizo kwa dua kali iliyosomwa na Abdurahman Ahmed, na Godlove Kivate.
Licha ya dua hiyo, Wambura aliihusia kamati ya uchaguzi itoe nafasi kwa wanachama wa klabu hiyo kuchagua viongozi wanaowataka.
“Wanachama wasikilize sera, uongozi ni dhamani hivyo kamati ya uchaguzi nayo iwape nafasi watu wachague viongozi wanaowataka,”alisema Wambura.
Wakati Wambura akiyasema hayo, Julio alitoa kali ya mwaka baada ya kusema anaidai million 24 viongozi wanaomaliza muda wake wake chini ya Mwenyekiti wake Ismail Aden Rage.
“Mimi bado ni kocha wa Simba kwa kuwa uongozi uliompindua Rage kikao chake kilikuwa sio haliali na mimi bado ni kocha halali wa timu hiyo.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Katibu msaidizi wa kamati ya Uchaguzi, Khalidi Kamguna alisema wagombea 41 wamechukua fomu kuwania uongozi wa timu hiyo.
Alisema kuwa zoezi hilo limefugwa jana ambapo kwa sasa watapitia fomu hizo zitapitiwa Mei 17 ambapo Mei 19 wagombea watatangazwa.
Aliwataja wagombea waliochukua fomu kwenye nafasi ya Rais ni Evans Aveva, Michael Wambura, na Andrew Tupa.
Makamu wa Rais waliochukua ni Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, Joseph Itang’are, Swedi Nkwabi, Bundara Kabulwa, Willbar Mayage na Julio.
![]() |
Jasmine Badawi naye amerejesha fomu |
![]() |
George Wakuganda naye amerejesha fomu |
![]() |
Asha Muhaji naye amerejesha fomu |
Wajumbe ni Abdulhamid Mshangama, Alfred Martin, Ally Sulu, Iddy.noor Kajuna, George Wakuganda, Said Tuli, Ramson Athuman, Seleiman Abdul, Khamis Mkom, Said Pamba, Rodney Chiduo.
Wengine ni, Collin Frisal, Chano Karaha, Emanuel Kazimoto, Juma Pinto, Salim Jazaa, Yassin Said, Hussein Simba, Damian Manembe, Ally Chaurembo, Ibrahim Masoud, Ahmed Mlanzi, Iddi Nassoro, Kessy Kikoti, Maulid Said, Juma Mussa, Omary Said, Said Kubenea.
Kamguna aliendelea kusema wanawake watatu wamejitokeza ni Asha kigundula, Asha Muhaji, Jasmin Badar na Amina Hussein.
0 comments:
Post a Comment