KOCHA wa Italia, Cesare Prandelli ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya Kombe la Dunia akimjumuisha mshambuliaji mtukutu, Mario Balotelli.
The Azzurri ipo Kundi D pamoja na England watakayoanza nayo mjini Manaus Juni 14, kana ya kucheza na Uruguay na Costa Rica.
Prandelli aliyekutana na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Januari mwaka huu visiwani Zanzibar, katika kikosi chake amemjumuisha mchezaji wa zamani wa Liverpool, Alberto Aquilani na Gabriel Paletta na atapunguza na kubaki na wachezaji 23 atakaokwenda nao Brazil.
![]() |
Kocha wa Italia, Prandelli alipokutana na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY, Mahmoud Zubeiry kulia visiwani Zanzibar Januari mwaka huu. Kocha huyo ametaja kikosi cha Italia Kombe la Dunia |
Ameitwa: Mshambuliaji wa AC Milan, Mario Balotelli amechukuliwa kwenye kikosi cha awali cha Italia, je atapona katika 23 wa mwisho?
KIKOSI CHA AWALI CHA ITALIA;
Makipa; Gianluigi Buffon (Juventus), Salvatore Sirigu (PSG), Mattia Perrin (Genoa)
Mabeki; Ignazio Abate (AC Milan), Andrea Barzagli (Juventus), Leandro Bonucci (Juventus), Giorgio Chiellini (Juventus), Matteo Darmian (Torino), Mattia De Sciglio (AC Milan), Christian Maggio (Lazio), Gabriel Paletta (Parma), Manuel Pasqual (Fiorentina), Andrea Ranocchia (Inter Milan)
Viungo; Alberto Aquilani (Fiorentina), Antonio Candreva (Lazio), Daniele De Rossi (AS Roma), Claudio Marchisio (Juventus), Riccardo Montolivo (AC Milan), Marco Parolo (Parma), Andrea Pirlo (Juventus), Thiago Motta (PSG), Romulo (Verona), Marco Verratti (PSG)
Washambuliaji; Mario Balotelli (AC Milan), Antonio Cassano (Parma), Alessio Cerci (Torino), Mattia Destro (AS Roma), Ciro Immobile (Torino), Lorenzo Insigne (Napoli), Giuseppe Rossi (Fiorentina)
0 comments:
Post a Comment