// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM TV YALETA KITU HICHO SHABIKI NAMBA MOJA ATAVUNA MILIONI 10 BAADA YA MWEZI MMOJA MJENGONI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM TV YALETA KITU HICHO SHABIKI NAMBA MOJA ATAVUNA MILIONI 10 BAADA YA MWEZI MMOJA MJENGONI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 20, 2014

    AZAM TV YALETA KITU HICHO SHABIKI NAMBA MOJA ATAVUNA MILIONI 10 BAADA YA MWEZI MMOJA MJENGONI

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    KAMPUNI ya Azam Media Group, kupitia Televisheni yake ya Azam TV, imeanzisha programu ya Kwetu House inayohusu shindano la mashabiki lijulikanalo kama Shabiki Namba Moja, ambalo mwisho wa siku, mshindi atajinyakulia kitita cha Sh. Milioni 10.
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington amewaambia Waandishi wa Habari katika Mkutano wa asubuhi ya leo makao makuu ya kampuni hiyo, eneo la Tazara, Dar es Salaam kwamba shindano hilo litahusisha mashabiki wa kiume pekee.
    Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Rhys Torrington kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo

    Muingereza huyo amesema kwamba utafanyika usaili kuanzia Jumamosi hii viwanja vya Leaders, Dar es Salaam na mwisho wa siku mashabiki 10 wa timu tofauti nchini wataingizwa kwenye nyumba moja kuzitetea klabu zao.
    “Yule ambaye atafanya vizuri zaidi katika jumba hilo, ndiye ambaye atakuwa mshindi na kuwa Shabiki Namba Moja, hivyo kujishindia Sh. Milioni 10,”amesema Torrington.
    Usaili wa kwanza utafanyika Jumamosi wiki hii Leaders Club, kuanzia Saa 3:00 asubuhi hadi Saa 11:00 jioni.
    Amesema mashabiki ambao hawatapata fursa ya kufika, wanaweza kutuma video zao kupitia namba 0759 386 568 kwa Whats App na zikikubalika wanaweza kupata nafasi ya kuingia kwenye nyumba ya Kwetu House, shindalo linalodhaminiwa na Azam Energy Drink.
    Torrington amesistiza shindano hilo ni kwa ajili ya mashabiki wa timu zote nchini na kigezo cha ushindi ni kufanya vizuri kwa shabiki katika kuitetea timu yake, bila kujali umaarufu au ukubwa wa timu hiyo.  









    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM TV YALETA KITU HICHO SHABIKI NAMBA MOJA ATAVUNA MILIONI 10 BAADA YA MWEZI MMOJA MJENGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top