• HABARI MPYA

    Wednesday, May 14, 2014

    ASHA KIGUNDULA AWAAMBIA SIMBA SC; “NINA UWEZO SANA TU”

    Na Baby Akwitende, Dar es Salaam
    ASHA Said Kigundula, ni mmoja wa wagombea wanawake wanne waliojitokeza kuwania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba inayotarajia kufanya uchaguzi Juni 29 mwaka huu.
    Wagombea wengine waliorejesha fomu kuwania nafasi hiyo moja ni Asha Muhaji, Jasmini Badir na Amina Poyo.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Kigundula, alisema kuwa anajiamini ana uwezo wa kuiongoza Simba.
    Asha Kigundula kulia akikabidhi fomu kwa Katibu wa Kamati ya uchaguzi, Khalid Kamguna kushoto
    Juma Pinto kulia akirejesha fomu leo


    Kigundula alisema kuwa moja ya sababu zilizomfanya achukue fomu ni kutaka kutoa mchango wake wa kuiendeleza klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi.
    "Naamini nina uwezo na Wanasimba wanatambua uwezo wangu,  nilianza kuitumikia Simba tangu nikiwa mdogo, hata mbuyu ulianza kama mchicha", alisema Kigundula.
    Alieleza kwamba huu ni wakati wa Simba kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua viongozi  watakaoisaidia klabu yao katika miaka minne ijayo.
    " Naomba nisiseme sana kwa sababu muda wa kampeni na kutangaza sera zetu haujafika", alisema mgombea huyo.
    Katika uchaguzi uliopita nafasi ya mwanamke ilibaki wazi kutokana na mgombea aliyekuwa amejitokeza kutokuwa na sifa na hivyo kuondolewa katika mchakato wa uchaguzi huo uliofanyika mwaka 2010.
    Moja ya mambo ambayo uongozi mpya unatakiwa kufanya ni kurejesha makali ya Simba ambayo haikuwa na matokeo mazuri katika misimu miwili iliyopita ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ASHA KIGUNDULA AWAAMBIA SIMBA SC; “NINA UWEZO SANA TU” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top