• HABARI MPYA

    Wednesday, May 14, 2014

    SAMATTA NA ULIMWENGU KUTUA DAR JUMAMOSI KUICHEZEA STARS DHIDI YA ZIMBABWE JUMAPILI

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    BAHATI ya aina yake. Washambuliaji wawili wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watawasili Jumamosi mchana kwa ajili ya kuichezea Taifa Stars dhidi ya Zimbabwe kuwania tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika Morocco mwaka 2015.  
    Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, amewasiliana na Mwenyekiti wa TPM, Moise Katumbi na amemuhakikishia Samatta na Uli watatua Dar es Salaam Jumamosi.
    Samatta kulia na Ulimwengu kushoto wakiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wiki iliyopita alipowatembelea DRC, vijana wanakuja kulitumikia taifa

    Awali, ilikuwa wachezaji hao wasije kabisa kwenye mechi hiyo kwa sababu klabu yao inawahitaji kwa mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Lakini kwa kuwa mchezo wa kwanza wa Kundi lao, A dhidi yao na El Hilal Omduran utachezwa Ijumaa mjini Khartoum nchini Sudan, Jumamosi wachezaji hao watapanda ndege kuja Dar es Salaam na kucheza mechi Jumapili Uwanja wa Taifa.
    Mara tu baada ya mwchi hiyo, wachezaji hao waterejea Lubumbashi DRC kwa maandalizi ya mchezo wa pili wa kundi lao dhidi ya AS Vita Mei 25, mwaka huu na baada ya hapo wanaweza kupata fursa ya kuja kwenda Zimbabwe kuchezea Stars mchezo wa marudiano. 
    Wazi kuja kwa wachezaji hao kuichezea Stars kunaongeza matumaini ya Stars kufanya vizuri, kwani Samatta na Ulimwengu kwa sasa ndio tegemeo la Tanzania. 
    Mshindi wa jumla kati ya Stars na Zimbabwe baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini, atapambana na mshindi kati ya Sudan Kusini na Msumbiji kuwania kuingia katika Kundi, rasmi kuanza mbio za Morocco 2015.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA NA ULIMWENGU KUTUA DAR JUMAMOSI KUICHEZEA STARS DHIDI YA ZIMBABWE JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top