• HABARI MPYA

    Friday, June 12, 2026

    MEXICO YAANZA VYEMA KOMBE LA DUNIA, YAICHAPA AFRIKA KUSINI 2-0


    WENYEJI, Mexico wameanza vyema Fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya ushindi wa mabao 2–0 dhidi ya Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi A usiku wa kuamkia jana Uwanja wa Azteca Jijini Mexico City.
    Katika mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki 80,824, mabao ya Mexico inayoandaa Fainali hizo kwa ushirikiano na majirani zake Canada na Marekani yalifungwa na winga wa Al-Qadsiah ya Saudi Arabia na Julián Andrés Quiñones Quiñones dakika ya tisa na mshambuliaji wa Wolverhampton Wanderers ya England, Raúl Alonso Jiménez Rodríguez dakika ya 67.
    Mechi nyingine ya kundi hilo itafuatia leo kuanzia Saa 11:00 Alfajiri kati ya Korea Kusini na Jamhuri ya Czech Uwanja wa Akron Jijini Zapopan.
    Wenyeji wengine, Canada watashuka Uwanja wa BMO Field Jijini Toronto kucheza mechi yao ya kwnza ya Kundi B dhidi ya Bosnia na Herzegovina kuanzia saa 4:00 usiku – wakati wenyeji wengine Marekani wao watatupa kete yao ya kwanza Kundi D kesho Saa 4:00 usiku watakapomenyana na Paraguay Uwanja wa SoFi Jijini Inglewood, Los Angeles County, California.

     

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MEXICO YAANZA VYEMA KOMBE LA DUNIA, YAICHAPA AFRIKA KUSINI 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top