TIMU ya Korea Kusini imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech katika mchezo wa Kundi A Fainali za Kombe la Dunia Alfajiri ya leo Uwanja wa Akron Jijini Zapopan, Jalisco nchini Mexico.
Mabao ya Korea Kusini yamefungwa na kiungo Hwang In-beom wa Feyenoord ya Uholanzi dakika ya 67 na mshambuliaji Oh Hyeon-gyu wa Beşiktaş ya Uturuki dakika ya 80, wakati bao pekee la Jamhuri ya Czech limefungwa na Nahodha wake, beki wa kati, Ladislav Krejcí anayecheza kwa mkopo Wolverhampton Wanderers ya England kutoka Girona ya Hispania dakika ya 59.
Ikumbukwe mechi ya kwanza ya kundi hilo usiku wa jana wenyeji, Mexico walianza vyema kwa ushindi wa mabao 2–0 dhidi ya Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi A usiku wa kuamkia jana Uwanja wa Azteca Jijini Mexico City.
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki 80,824, mabao ya Mexico inayoandaa Fainali hizo kwa ushirikiano na majirani zake Canada na Marekani yalifungwa na winga wa Al-Qadsiah ya Saudi Arabia na Julián Andrés Quiñones Quiñones dakika ya tisa na mshambuliaji wa Wolverhampton Wanderers ya England, Raúl Alonso Jiménez Rodríguez dakika ya 67.
Wenyeji wengine, Canada watashuka Uwanja wa BMO Field Jijini Toronto kucheza mechi yao ya kwnza ya Kundi B dhidi ya Bosnia na Herzegovina kuanzia saa 4:00 usiku – wakati wenyeji wengine Marekani wao watatupa kete yao ya kwanza Kundi D kesho Saa 4:00 usiku watakapomenyana na Paraguay Uwanja wa SoFi Jijini Inglewood, Los Angeles County, California.

.png)
0 comments:
Post a Comment