• HABARI MPYA

    Saturday, June 13, 2026

    BALOGUN APIGA MBILI MAREKANI YAILAMBA PARAGUAY 4-1 KOMBE LA DUNIA


    WENYEJI, Marekani wameibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-1 dhidi ya  Paraguay katika mchezo wa Kundi D Fainali za Kombe la Dunia Alfajiri ya leo Uwanja wa SoFi Jijini Inglewood, Los Angeles County, California.
    Mabao ya USA yamefungwa na kiungo wa Sao Paulo ya Brazil, Damián Josué Bobadilla Benítez aliyejifunga dakika ya saba, mshambuliaji wa Monaco ya Ufaransa, Folarin Jerry Balogun aliyefunga mawili dakika ya 31 na 45’+5 na kiungo mshambuliaji wa Borussia Mönchengladbach ya Ujerumani, Giovanni Alejandro Reyna dakika ya 90’+8.
    Bao pekee na la kufutia machozi la Paraguay katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mholanzi, Danny Makkelie mbele ya mashabiki 70,492 limefungwa na kiungo wa Palmeiras ya Italia, Maurício Magalhaes Prado dakika ya 73.
    Mchezo mwingine wa Kundi C utafuatia Saa 1:00 Asubuhi ya kesho kati ya Australia  na Uturuki Uwanja wa BC Place Jijini Vancouver nchini Canada. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BALOGUN APIGA MBILI MAREKANI YAILAMBA PARAGUAY 4-1 KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top