MSHAMBULIAJI Wayne Rooney atakosa mechi ya mwisho ya msimu ya timu yake, Manchester United nyumbani dhidi ya Hull City kutokana na maumivu ya nyonga.
Rooney alikuwa nje United ikipigwa 1-0 na Sunderland mwishoni mwa wiki kutokana na majeruhi hayo pamoja na kuumwa tumbo.
Kocha wa muda na mchezaji wa timu hiyo,Ryan Giggsamesema kuelekea mchezo huo dhidi ya Hull kwamba, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 bado hajapona maumivu yake.
0 comments:
Post a Comment