Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
NYOTA waliowahi kuwika katika klabu ya Real Madrid ya Hispania, watafanya ziara nchini Tanzania Agosti mwaka huu- na mmoja wa wachezaji wa zamani wa timu hiyo Ruben de la Red alitua nchini mapema mwezi huu kuja kuthibitisha ziara hiyo.
Ruben ambaye ni Nahodha timu ya magwiji yaReal Madrid, aliambatana na mchezaji mwingine mkongwe Rayo Garcia pamoja na Ofisa wa Idara ya Habari ya Real Madrid na akasema katika ziara yao watakuja na magalctico 25.
“Tutakuwa hapa kwa ziara ya siku tatu, mbali ya mechi ya kirafiki (Agosti 23 na Taifa Stars), pia tutatembelea mbuga za wanyama na vivutio mbalimbali vya kiutalii, nafikiri tutapanda mlima Kilimanjaro,”alisema De la Red akizungumza na BIN ZUBEIRY mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Dar es Salaam.
Timu hiyo inakuja nchini kwa mwaliko wa makampuni ya TSN, chini ya Mkurugenzi wake Mtendaji, Farough Baghoza ambaye Jumapili iliyopita alitiliana saini Mkataba wa ziara hiyo na Ruben De La Red.
Nyota wa zamani wa Real, kama Ronaldo Lima, David Beckham, Luis Figo, Zinadine Zidane na wengine wanatarajiwa kuwamo katika ziara hiyo ya kihistoria nchini.
RUBEN DE LA RED NI NANI?
Kama si matatizo ya moyo, kijana huyo mdogo aliyezaliwa Juni 5, mwaka 1985 hadi leo angekuwa anaendelea kucheza katika nafasi yake ya kiungo cha kati.
Alijipatia jina alipokuwa klabu ya Getafe baada ya kuibukia katika timu ya vijana ya Real Madrid kabla ya kurejea katika klabu yake ya awali mwaka 2008.
Hata hivyo, De La Red hakuweza kuendelea na soka licha ya kuwa na kipaji, kwani matatizo ya moyo yalimlazimisha kustaafu mwishoni mwa mwaka 2010 baada ya kusimama kucheza kwa miaka miwili.
De la Red alikuwemo kwenye kikosi cha Hispania kilichotwaa Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2008.
Alizaliwa mjini Mostoles, eneo la Madrid na alitua katika akademi ya Real Madrid akiwa na umri wa miaka 14, hata hivyo wakati huo akapelekwa
CD Mostoles baada ya kuambiwa hana kiwango, lakini baada ya muda mdupi akarejeshwa Madrid. Baada ya msimu wake wa nne akiwa na timu ya akademi, kocha Quique Flores, aliyehamia Getafe CF, alimtaka mchezaji huyo aondoke naye katika klabu yake mpya, lakini Madrid ikamkatalia.
De la Red alichezea kikosi cha kwanza cha Real kwa mara ya kwanza Novemba 10, mwaka 2004 ikishinda 2–1 ugenini dhidi ya CD Tenerife katika mchezo wa Kombe kla Mfalme.
Mechi yake ya kwanza ya La Liga alicheza Septemba 22 mwaka 2005, akicheza kwa dakika mbili katika ushindi wa nyumbani wa 3–1 dhidi ya Athletic Bilbao na baada ya hapo akacheza mechi mbili zaidi akitokea benchi msimu huo.
Msimu wa 2006–07 de la Red aliingizwa rasmi kikosi cha kwanza na kocha wa wakati huo, Fabio Capello, sambamba na wachezaji wenzake Miguel Torres na Miguel Angel Nieto, ambako alifanikiwa kucheza mechi saba katika msimu huo Real ikitwaa ubingwa. Alifunga bao lake la kwanza akichezea kikosi cha kwanza Novemba 9, mwaka 2006 dhidi ya Ecija Balompie katika mechi ya Kombe la Mfalme, Real ikishinda 5–1 nyumbani na kuwatoa wapinzani wao kwa ushindi wa jumla wa 6–2.
Haikuwa ajabu kwa mafanikio hayo Julai mwaka 2007, akapewa Mkataba mpya ambao ulitarajiwa kumalizika mwaka 2011.
Agosti 31, mwaka 2007 de la Red alihamishiwa kwa maswahiba zao, Getafe, huku Real Madrid ikiwa na nafasi ya kumnunua tena ndani ya miaka miwili. Huko ndiko, ambako alitengeneza jina haswa akiwa mchezaji wa kikosi cha kwanza kiasi cha hadi kuitwa timu ya taifa ya Hispania.
Katika msimu huo, kuna wakati alilazimika kucheza beki ya kati baada ya timu hiyo kukumbwa na balaa la majeruhi na moja ya mechi za kukumbukwa alizocheza nafasi ya ulinzi ni Robo Fainali ya Kombe la UEFA dhidi ya FC Bayern Munich, ambayo katika mchezo wa marudiano alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya sita.
Katika michuano hiyo ya Ulaya, alifunga mabao matatu kwenye mechi 11, ikiwemo waliyoshinda 2–1 dhidi ya Tottenham Hotspur Oktoba 25, mwaka 2007, akisawazisha baada ya kugongeana vizuri na Granero.
Rais wa Real Madrid, Ramon Calderon alithibitisha Mei mwaka 2008 kwamba, pamoja na Granero na Javi Garcia, de la Red atarajea Santiago Bernabeu kwa msimu wa 2008–2009.
Ilipendekezwa wakati huo atabadilishwa kwa mchezaji kutoka timu nyingine, lakini kocha Bernd Schuster akasema kwamba yuko tayari kumpa nafasi kiungo huyo katika timu ya kwanza.
De la Red akafunga bao lake la kwanza tangu arejee Agosti 24, mwaka 2008, katika mchezo wa marudiano wa Super Cup ya Hispania dhidi ya Valencia CF, kwa shuti kali la mbali, hivyo kupangwa katika mchezo mwingine wa Ligi, ambao ulikuwa wa kwanza kwake tangu arejee Real –Septemba 21 dhidi ya Racing de Santander timu hiyo ikishinda 2-0 ugenini.
Oktoba 30, mwaka 2008, de la Red alilazwa hospitali baada ya kuzimia uwanjani katika mchezo wa Kombe la Hispania dhidi ya Real Union na Desemba 12 klabu hiyo ikatangaza mchezaji huyo atakosa sehemu iliyobaki ya msimu akipata matibabu ya moyo.
Mwishoni mwa mwaka 2009, baada ya kufanyiwa vipimo vya kina, ikathibitishwa de la Red atakosa msimu wote wa 2009–2010, na akapangiwa ratiba ya kuhudhuria hospitali kwa vipimo kila baada ya miezi miwili.
Julai 2, klabu hiyo ikatangaza kumsaini mchezaji mpya, Raul Albiol aliyepewa jezi namba 18, ambayo awali ilikuwa inavaliwa na de la Red, na beki huyo akaahidi kuirejesha jezi hiyo kwa mwenyewe atakapopona na kurejea uwanjani.
Januari mwaka 2010, iliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari Madrid kwamba, Real Madrid imekiri tatizo la moyo la de la Red ni sugu na wanatafuta namna ya kuubadili Mkataba wake.
Kwa sababu hiyo, mchezaji huyo akawa analipwa Euro 1,500 kwa mwezi, kuliko kupewa mshahara mzima katika miaka miwili ilyobaki kwenye Mkataba wake.
Novemba 3, mwaka 2010, de la Red alitangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 25 tu na kabla ya kutangaza hilo, alisema atabaki katika klabu kama kocha wa akademi.
Mkurugenzi wa Soka, Jorge Valdano – ambaye pia ni mchezaji wa zamani na kocha, alisema Ruben anastaafu soka na anaelekeza nguvu zake katika ukocha. “Kuanzia leo, yeye ni sehemu ya makocha wa Real Madrid na ataanza kusoma. Pia atakuwa sehemu ya wasaidizi wa Mourinho”alisema.
Katika soka ya kimataifa, De la Red alichezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Hispania kabla ya kupandishwa katika timu ya wakubwa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia Machi 26, mwaka 2008, lakini hakupangwa.
Akiwa hajaichezea hata mechi moja timu ya taifa, aliitwa katika kikosi cha wachezaji 22 wa kwenda Euro 2008 chini ya kocha Luis Aragones, na kuingia kwenye ratiba ya mechi za kupasha kabla ya michuano hiyo dhidi ya Peru na Marekani.
Katika mchezo wa mwisho wa makundi, de la Red alifunga bao lake pekee katika mechi za kimataifa dhidi ya Ugiriki Juni 18, Hispania ikishinda 2–1.
Kama ulikuwa humjui, basi huyo ndiye Ruben de la Red ambaye kwa sasa ni kocha Mkuu wa akademi ya Real na Nahodha wa timu ya magwiji ya Real Madrid.
NYOTA waliowahi kuwika katika klabu ya Real Madrid ya Hispania, watafanya ziara nchini Tanzania Agosti mwaka huu- na mmoja wa wachezaji wa zamani wa timu hiyo Ruben de la Red alitua nchini mapema mwezi huu kuja kuthibitisha ziara hiyo.
![]() |
| Magalctico; Ruben de la Red kushoto akiwa na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Blog mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Dar es Salaam alipokuja kusaini Mkataba wa ujio ya magwiji wa timu hiyo |
![]() |
| Ruben de la Red akishangilia bao lake dhidi ya Ugiriki katika Euro 2008 |
Timu hiyo inakuja nchini kwa mwaliko wa makampuni ya TSN, chini ya Mkurugenzi wake Mtendaji, Farough Baghoza ambaye Jumapili iliyopita alitiliana saini Mkataba wa ziara hiyo na Ruben De La Red.
Nyota wa zamani wa Real, kama Ronaldo Lima, David Beckham, Luis Figo, Zinadine Zidane na wengine wanatarajiwa kuwamo katika ziara hiyo ya kihistoria nchini.
![]() |
| Ruben de la Red enzi zake Real Madrid akishangilia moja ya mabao aliyofunga |
RUBEN DE LA RED NI NANI?
Kama si matatizo ya moyo, kijana huyo mdogo aliyezaliwa Juni 5, mwaka 1985 hadi leo angekuwa anaendelea kucheza katika nafasi yake ya kiungo cha kati.
Alijipatia jina alipokuwa klabu ya Getafe baada ya kuibukia katika timu ya vijana ya Real Madrid kabla ya kurejea katika klabu yake ya awali mwaka 2008.
Hata hivyo, De La Red hakuweza kuendelea na soka licha ya kuwa na kipaji, kwani matatizo ya moyo yalimlazimisha kustaafu mwishoni mwa mwaka 2010 baada ya kusimama kucheza kwa miaka miwili.
De la Red alikuwemo kwenye kikosi cha Hispania kilichotwaa Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2008.
Alizaliwa mjini Mostoles, eneo la Madrid na alitua katika akademi ya Real Madrid akiwa na umri wa miaka 14, hata hivyo wakati huo akapelekwa
CD Mostoles baada ya kuambiwa hana kiwango, lakini baada ya muda mdupi akarejeshwa Madrid. Baada ya msimu wake wa nne akiwa na timu ya akademi, kocha Quique Flores, aliyehamia Getafe CF, alimtaka mchezaji huyo aondoke naye katika klabu yake mpya, lakini Madrid ikamkatalia.
De la Red alichezea kikosi cha kwanza cha Real kwa mara ya kwanza Novemba 10, mwaka 2004 ikishinda 2–1 ugenini dhidi ya CD Tenerife katika mchezo wa Kombe kla Mfalme.
Mechi yake ya kwanza ya La Liga alicheza Septemba 22 mwaka 2005, akicheza kwa dakika mbili katika ushindi wa nyumbani wa 3–1 dhidi ya Athletic Bilbao na baada ya hapo akacheza mechi mbili zaidi akitokea benchi msimu huo.
Msimu wa 2006–07 de la Red aliingizwa rasmi kikosi cha kwanza na kocha wa wakati huo, Fabio Capello, sambamba na wachezaji wenzake Miguel Torres na Miguel Angel Nieto, ambako alifanikiwa kucheza mechi saba katika msimu huo Real ikitwaa ubingwa. Alifunga bao lake la kwanza akichezea kikosi cha kwanza Novemba 9, mwaka 2006 dhidi ya Ecija Balompie katika mechi ya Kombe la Mfalme, Real ikishinda 5–1 nyumbani na kuwatoa wapinzani wao kwa ushindi wa jumla wa 6–2.
![]() |
| Ruben de la Red akimkabidhi Rais wa TFF, Jamal Malinzi jezi ya Real Madrid |
Agosti 31, mwaka 2007 de la Red alihamishiwa kwa maswahiba zao, Getafe, huku Real Madrid ikiwa na nafasi ya kumnunua tena ndani ya miaka miwili. Huko ndiko, ambako alitengeneza jina haswa akiwa mchezaji wa kikosi cha kwanza kiasi cha hadi kuitwa timu ya taifa ya Hispania.
Katika msimu huo, kuna wakati alilazimika kucheza beki ya kati baada ya timu hiyo kukumbwa na balaa la majeruhi na moja ya mechi za kukumbukwa alizocheza nafasi ya ulinzi ni Robo Fainali ya Kombe la UEFA dhidi ya FC Bayern Munich, ambayo katika mchezo wa marudiano alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya sita.
Katika michuano hiyo ya Ulaya, alifunga mabao matatu kwenye mechi 11, ikiwemo waliyoshinda 2–1 dhidi ya Tottenham Hotspur Oktoba 25, mwaka 2007, akisawazisha baada ya kugongeana vizuri na Granero.
Rais wa Real Madrid, Ramon Calderon alithibitisha Mei mwaka 2008 kwamba, pamoja na Granero na Javi Garcia, de la Red atarajea Santiago Bernabeu kwa msimu wa 2008–2009.
Ilipendekezwa wakati huo atabadilishwa kwa mchezaji kutoka timu nyingine, lakini kocha Bernd Schuster akasema kwamba yuko tayari kumpa nafasi kiungo huyo katika timu ya kwanza.
De la Red akafunga bao lake la kwanza tangu arejee Agosti 24, mwaka 2008, katika mchezo wa marudiano wa Super Cup ya Hispania dhidi ya Valencia CF, kwa shuti kali la mbali, hivyo kupangwa katika mchezo mwingine wa Ligi, ambao ulikuwa wa kwanza kwake tangu arejee Real –Septemba 21 dhidi ya Racing de Santander timu hiyo ikishinda 2-0 ugenini.
Oktoba 30, mwaka 2008, de la Red alilazwa hospitali baada ya kuzimia uwanjani katika mchezo wa Kombe la Hispania dhidi ya Real Union na Desemba 12 klabu hiyo ikatangaza mchezaji huyo atakosa sehemu iliyobaki ya msimu akipata matibabu ya moyo.
Mwishoni mwa mwaka 2009, baada ya kufanyiwa vipimo vya kina, ikathibitishwa de la Red atakosa msimu wote wa 2009–2010, na akapangiwa ratiba ya kuhudhuria hospitali kwa vipimo kila baada ya miezi miwili.
Julai 2, klabu hiyo ikatangaza kumsaini mchezaji mpya, Raul Albiol aliyepewa jezi namba 18, ambayo awali ilikuwa inavaliwa na de la Red, na beki huyo akaahidi kuirejesha jezi hiyo kwa mwenyewe atakapopona na kurejea uwanjani.
Januari mwaka 2010, iliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari Madrid kwamba, Real Madrid imekiri tatizo la moyo la de la Red ni sugu na wanatafuta namna ya kuubadili Mkataba wake.
Kwa sababu hiyo, mchezaji huyo akawa analipwa Euro 1,500 kwa mwezi, kuliko kupewa mshahara mzima katika miaka miwili ilyobaki kwenye Mkataba wake.
Novemba 3, mwaka 2010, de la Red alitangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 25 tu na kabla ya kutangaza hilo, alisema atabaki katika klabu kama kocha wa akademi.
Mkurugenzi wa Soka, Jorge Valdano – ambaye pia ni mchezaji wa zamani na kocha, alisema Ruben anastaafu soka na anaelekeza nguvu zake katika ukocha. “Kuanzia leo, yeye ni sehemu ya makocha wa Real Madrid na ataanza kusoma. Pia atakuwa sehemu ya wasaidizi wa Mourinho”alisema.
Katika soka ya kimataifa, De la Red alichezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Hispania kabla ya kupandishwa katika timu ya wakubwa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia Machi 26, mwaka 2008, lakini hakupangwa.
Akiwa hajaichezea hata mechi moja timu ya taifa, aliitwa katika kikosi cha wachezaji 22 wa kwenda Euro 2008 chini ya kocha Luis Aragones, na kuingia kwenye ratiba ya mechi za kupasha kabla ya michuano hiyo dhidi ya Peru na Marekani.
Katika mchezo wa mwisho wa makundi, de la Red alifunga bao lake pekee katika mechi za kimataifa dhidi ya Ugiriki Juni 18, Hispania ikishinda 2–1.
Kama ulikuwa humjui, basi huyo ndiye Ruben de la Red ambaye kwa sasa ni kocha Mkuu wa akademi ya Real na Nahodha wa timu ya magwiji ya Real Madrid.

.png)
0 comments:
Post a Comment