KINDA wa umri wa miaka 18, James Anthony Wilson usiku huu
ameifungia Manchester United mabao mawili ikishinda 3-1 katika mchezo wa Ligi
Kuu ya England, Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester dhidi ya Hull City.
Bwana mdogo huyo alifunga bao la kwanza dakika ya 31 na la pili
dakika ya 61, wakati bao la Hull City lilifungwa na Matt Fryatt dakika ya 63
kabla ya Robin van Persie kuwafungia Mashetani Wekundu la tatu dakika ya 86.
Watoto tunaweza; Kinda James Wilson akishangilia baada ya kufunga usiku huu |
Ushindi huo, unaifanya United itimize pointi 63 baada ya kucheza
mechi 36, ikiendelea kubaki nafasi ya saba nyuma ya Tottenham Hotspur yenye
pointi 66 za mechi 37.
Kocha wa muda wa United, Ryan Giggs leo kwa mara ya kwanza
alicheza tangu aanze kukaimu nafasi ya David Moyes wiki mbili zilizopita,
akiingia kuchukua nafasi ya Thomas Lawrence dakika ya 70 sawa na Nemanja Vidic aliyempokea
Phil Jones dakika ya 22 na Van Persie aliyemrithi Wilson dakika ya 64.
0 comments:
Post a Comment