• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 03, 2010

  MISS KINONDONI 2010


  DAR Indian Ocean imeendelea kutamba katika Miss Kinondoni, baada ya juzi kushika nafasi mbili za ujuu kwenye shindano hilo, lililofanyika ukumbi wa MIimani City, Dar es Salaam.
  Alice Lushiku ndiye aliyetwaa taji la Miss Kinondoni, nafasi ya pili ikienda kwa Amisuu Malick na watatu alikuwa ni Irene Hezron. Kwa ushindi huo, Alice alizawadiwa fedha taslimu Sh Milioni 1.5, Amisuu Milioni 1 na Irene Hezron Sh. 800,000 sambamba na wote kupata tiketi uya kushiriki Miss Tanzania mwaka huu.
  Alice mbali na kuwa Miss Kinondoni, pia alijinyakulia taji la mrembo mwenye kipaji na kuzawadiwa Sh. 500,000, hivyo kuondoka na jumla ya Sh. Milioni 2.
  Edna Kwilasa aliyeshika nafasi ya nne Calorine Ndembo aliyekuwa wa tano, kila mmoja alipewa Sh. 300,000, wakati washiriki wengine walipata kifuta jasho cha Sh.150,000 kila mmoja. Hao ni Tamara Ally, Mwanaidi Nuhu, Salma Ally, Happy Andrew, Nuria Ahmed na Nancy Errol,
  Shindano hilo lililoandaliwa na Boy George Promotion, lilipambwa na burudani ya THT na sebene la African Stars ‘Twanga Pepeta’ lililoporomoshwa na wanenguaji wake mahiri akina Super Nyamwela, Queen Suzy na Sabrina.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MISS KINONDONI 2010 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top